Wednesday, 13 December 2017

Urithi wa watumishi wa Mungu

URITHI WA WATUMISHI WA MUNGU.

------------------------------------------------------------

Hii wengi hawafahamu lakini leo fahamu japo kiduchu. Ni kwa faida yako uchaguwe either umtumikie Mungu kwa kumaanisha au ufanye pritendinding.

But usije ukaja sema sikukwambia " kupretend kumtumikia Mungu ni hasara  kubwa sana. Ni kupoteza mda sana.

But my Friend fahamu hili  kumtumikia Mungu kunafaida nyingi sana. Zipo faida nyingi sana hapa duniani na uhakika wa uzima wa milele na kupewa thawabu na Bwana.  Pia My friend kuna karamu ya Mwanakondoo pamoja na Bwana na Maandaliza yamekamilika.

Hili naomba ufahamu ili tusije sikia kesho umefungua kanisa ukifilia kumtumikia Mungu ni kuwa Mchunga tu au kuwa na kanisa. Kumtumikia Mungu ni zaidi ya kuwa mhubiri au mchungaji.  Next time ntaeleza kwa kirefu.

Leo nakupa hizi Mbili Muhimu sana.

Neno linasema...
" Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio #urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana."- Isaya 54:17

¶- Hakuna silaha itakayo fanikiwa juu ya Mtumishi. { Siraha}
      ~Yes neno halijasema hakuna siraha itayo tumwa kwa watumishi zipo tena nyingi sana na kwa kadri utakavyo inuliwa na siraha zinakuwa nzito nzito. Lakini  Hakuna itakayo fanikiwa.

¶- Watakao kuhukumu mkosa utawahukumu wakosa. { Ndimi}
    ~ Yes Zipo ndimi ziinukazo kunena mabaya zidi ya watumishi wa Mungu.  Na kwakujua hili Mungu aliachilia uweza juu ya watumishi kuzihuku ndimi zinazo wahukumu.   So ukisikia kunamtu alimuhukumu Mtumishi kisha hukumu ileile imempata iko hivi.

Inawezekana wewe ni mtumishi lakini haujui hii siri.  Fahamu leo.  Neno linasema…
" Tena mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru” ~Yohana 8:32)

Leo macho yako yametiwa nuru.

Amani ya Mungu iwe nawe.

Ubarikiwe.

Minister: Enoch Joseph
Life word Ministry
Dar es salaam.
★2017

Walio vipofu rohoni wapate kuona na walio viziwi rohoni wapate kusikia.

Walio vipofu rohoni wapate kuona na walio viziwi rohoni wapate kusikia.

________________

Neno linasema...

"  Sikilizeni, enyi viziwi; tazameni, enyi vipofu, mpate kuona."
             ~Isaya 42: 18

Mungu aliweka Macho ya rohoni kwa kila mwanadamu na kazi yake ilikuwa waone rohoni. Macho ya utu wa ndani yapate kuona kwa jinsi ya rohoni. Lakini wengi ni vipofu rohoni na hawajuwi kuwa ni vipofu na haiwasumbui kitu wao kuwa vipofu kwasababu Hawajui kuwa wao ni vipofu. Na ivyo hawaombi Mungu awafunguwe Macho ya Ndani kwa sababu hawajui kuwa wanayaitaji ili wafanikiwe na kupiga hatua vizuri katika maisha ya rohoni na Mwilini.

Watu wengi sana ni viziwi wa rohoni na wachache sana wanajuwa kuwa wao ni viziwi. na kwasababu hawajuwi kuwa ni viziwi hawapati tabu wala kujisumbuwa na kumwomba Mungu wapone wapate kusikia. Na hii ni kwasababu hawajui kwamba hawajui kuwa wao ni viziwi. Na hawajui kwamba kufanikiwa kwao katika eneo lolote la maisha yao hapa duniani wanaitaji imani ambayo huja kwa kusikia.

Umebarikiwa wewe usomaye na kusikia ya kwamba Ni mpango wa Mungu uone na nimpango wa Mungu usikie.

Kwa Jina la Yesu upate kusikia ewe uliye kiziwi.
Kwa Jina la Yesu upate kuona wewe uliye kipofu.

Amen.
Imekuwa.

______________________

Minister: Enoch Joseph
Life word Teaching Ministry
★2017.

Nawezaje kuacha kuihubiri injiri ya Yesu. Maana ni kama moto uwakao ndani ya mifupa yangu wala siwezi kujizuia

Nawezaje kuacha kuihubiri injiri ya Yesu. Maana ni kama moto uwakao ndani ya mifupa yangu wala siwezi kujizuia

Neno linasema...

"  Nami nikisema, Sitamtaja( Hubiri na kufundisha neno la Mungu), wala sitasema tena kwa jina lake; basi, ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia."
                ~Yeremia 20: 9.

" But if I say I’ll never mention the Lord or speak in his name, his word burns in my heart like a fire. It’s like a fire in my bones! I am worn out trying to hold it in! I can’t do it!"

I will Teach the word of God

in Church
in Facebook
in Twitter
in YouTube
in Radio
in Tv Station
in Public
in office
in school
in part of the world. etc.

To day
This Year 2017, The coming Year and all the days of my life.

Nothing will stop me to do what God LOVE.

______________________

    Minister: Enoch Joseph
Life word Teaching  Ministry
        ★2017

Sifa ya Mtumishi wa Mungu.

Moja ya sifa kubwa ya Mtumishi wa Mungu anapaswa kuwa msiri.
__________________________

Neno linasema...

 "Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu"
       ~1cor 4:1
__________________________

Nikiwa katika tafakari ya neno Mungu Roho mtakatifu akanionesha kitu.

wapendwa wengi sio wasiri wa Mungu  na ndiyo maana kwa kadri wanavyo endelea kukomaa na tabia Hii Kiwango cha Mungu kuwaamini kinapunguwa na ishara ya kuwa hawaaminiki mbele za Mungu. Mungu huacha au hupunguza kuwapa siri za Mbinguni. kwani kutokuwa msiri ni sawa na kusema umekosa kigezo au sifa cha kuwa mtumishi wa Mungu.

wapendwa wengi ukiwakuta wanaongea utakuta wanamwaga siri za Watu hadharani. kisha hujifariji kwakuambiana ni siri. na kila atakaye sambaza huendelea kusema ni siri. mpaka neno siri linapoteza maana yake.

Mungu kuwaruhusu watu wajekwako mtu wa Mungu waeleza mambo yao ya siri ni kutokana na Mungu kukuamini.

sikumoja Yesu aliwaponya watu kisha akawaambia wasiseme kisha wakasema na kueneza mjimzima.

Neno linasema...

"  Naye alipofika nyumbani, wale vipofu walimwendea; Yesu akawaambia, Mnaamini kwamba naweza kufanya hili? Wakamwambia, Naam, Bwana.Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate. Macho yao yakafumbuka. Naye Yesu akawaagiza kwa nguvu, akisema, Angalieni hata mtu mmoja asijue.Lakini wakatoka, wakaeneza habari zake katika nchi ile yote."

            ★~Mathayo 9: 28-31

Kumbe ukioneshwa na Mungu jambo ambalo ni siri usimwambie mtu kaa kimya.

hawajamaa Yesu kawa ponya walikuwa vipofu.
lakini wakashidwa kutenda kama alivyo waamuru kwa nguvu. Kweli kuwa mtumishi wa sio jambo jepesi.

Na ukitaka habari ienee mji mzima waambie ni siri..

#Siri

__________________

     Minister: Enoch Joseph
  Life word Teaching Ministry
           ★2017

Mshukuru Mungu

Unafanyaje Mungu akikutendea kitu. Unapaswa kumshukuru Mungu.

Neno linasema...

"  Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao."
            ~ Mathayo 8: 4.

Yesu alipo mponya Mtu Mwenye ukoma akampa maelekezo ya msingi ambayo anapaswa afanye.

                       
#A- Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani.
     - Mathayo 9:28-31. aliwaponya wenye upofu kisha aka waambia mtu yeyote asijuwe lakini wao wakaeneza habari zile kila mtu akajuwa. Kwahiyo alipo sema usimwambie mtu ilikuwa ni jambo moja but condition ya msingi ilikuwa nenda ukajioneshe kwa Kuhani.
     Swali Yesu akikuponya unaenda kujionesha kwa nani?  Pengine unaweza sema Yesu amekuponya kupitia huyo kuhani. Bado swali ni Je umeenda kujionesha kwake na kumshuhudia Bwana Yesu aliyo tenda kupitia Yeye.

★ Kumbuka kwa kuhani Kuna ulinzi unapoenda kwa kuani kujionesha unaripoti kwa mlinzi achukuwe zamu ya ulinzi.
         Ndiyo maana neno linasema...
" Nimeweka walinzi( Kuhani)  juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya;"
             ~Isaya 62: 6.
NB. Kumbuka kuhani wa Bwana anaweza kuwana cheo cha.
     i- Mtume
    ii-Nabii
   iii-Mwinjiristi.
   iv- Mchungaji
   v- Mwalimu.

Yesu akamwambia akajioneshe kwa Kuhani.

#B. Ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.
      Kumbe unapo enda kujionesha kwa Kuhani unapaswa kuwa na sadaka kama alivyoamuru Musa. Kumbuka haya ni Maneno ya Yesu.

Sadaka utakayo itoa itakuwa ushuhuda kwao. Ushuhuda wako utaambatana na sadaka. Kwa lugha nyepesi sadaka yako itakuwa ushuhuda kwa Kuhani. sadaka hubeba ushuhuda.

Kumbuka Mungu akikutendea jambu Neno shukrani kwa Mungu lisikosekane kwako.

Linda Muujiza wako kwa kumshukuru Mungu
Tengeneza Muujiza mwingine kwa kumshukuru Mungu.

Amen.

Ubarikiwe na Yesu.

_________________________

Minister: Enoch Joseph
Life word Teaching Ministry
★2017.

Furahini sikuzote.

Bwana asema...

"... wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu."
       ★~Nehemia 8: 10.

~Sikia neno la Bwana  usihuzunike.
   Huzuni huondoa nguvu.

~Furaha ya Bwana ndiyo Nguvu yako.

Ni maombi yangu Furaha ya Bwana iwe pamoja nawe haijalishi mahali unapitia. Huzuni uliyo nayo Bwana Yesu aichukuwe na Umpatie huzuni yako. Furaha ya Bwana iwe pamoja nawe na Maana ndiyo Nguvu zako.

Ubarikiwe.

______________

Minister: Enoch Joseph
Life word Teaching Ministry.
    ★2017.

Wednesday, 18 October 2017

DAMU YA YESU INAVYOWEZA KUKUTOA ULIPOKWAMISHWA NA URITHI MBAYA

SEMINA YA NENO LA MUNGU UWANJA WA TANGANYIKA PACKERS - DAR ES SALAAM

MWL.CHRISTOPHER MWAKASEGE

TAREHE 15 OKTOBA 2017

*SIKU YA NANE*
*👉NAMBA ZA SADAKA*
http://www.mwakasege.org/kuchangia.htm
*👉KUSIKILIZA MAOMBI PALE MWISHONI BONYEZA MAANDISHI HAYA* https://drive.google.com/…/0B3OfNJtOXYXuLWdEYW9GLXV3a…/view…
*👉LINK YA SEMINA YA LEO YOUTUBE*. SUBSCRIBE Youtube channel ya Mwalimu Christopher Mwakasege uweze kupata updates na alert za semina na masomo mapya
https://youtu.be/b1RAlWUOYhc
*👉KUPATA CD & DVDs ZA SOMO HILI.*
Hii ni summary ya siku ya nane ya somo hili hapa Dar es Salaam. Tembelea www.mwakasege.org kupata maelezo zaidi na kununua Kanda, CDs ama DVDs za siku zote kuanzia siku ya kwanza ili uweze kupata undani wa somo hili. Cd za semina hii zinapatikana *Luther house ghorofa ya tatu karibu na kanisa la KKKT AZANIA FRONT POSTA ( DAR ES SALAAM) au wasiliana na Dina 0754766517*
*Note: Pia unaweza ukasoma vizuri zaidi kwa google plus, Copy hili somo na paste na post google+ kwenye account yako utasoma vizuri na utaona bold na italic kama huoni hapa whatsapp*
*LENGO LA SOMO*.
_*Kuweza kutumia DAMU YA YESU ili uweze kujitoa katika urithi mbaya.*_
Leo nataka tuangalie
*FAIDA ZA KUIMARISHA IMANI YAKO BINAFSI KIMATENDO JUU YA DAMU YA YESU*
Ili iweze kukusaidia kushughulika na urithi mbaya unaokwamisha maisha yake.
*WARUMI 3:23-26*
_“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake, ili aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa; apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu.”_
Nataka uone neno kwa imani katika DAMU yake. Tafsiri ya neno *njia* kibiblia maana yake ni _*mkakati yaani strategy.*_ Kwa hiyo anaposema mawazo yangu si mawazo yenu au njia zangu si njia zenu anataka kutuambia juu ya mkakati wa kukufikisha mahali. Hazungumzii tu njia kama ya kupita.
Kwa hiyo MUNGU anaposema njia itazame kwa jicho pana kidogo, kwa hiyo unaposikia jinsi gani kijana aisafishe njia [mkakati] yake ni kwa kutii na kwa kufuata neno la MUNGU.
Kwa hiyo maandiko yanaposema “kwa njia ya imani katika damu yake, angalia kwa upana kidogo au nenda na tafsiri hii *“kuna njia ya au mkakati wa imani katika DAMU YA YESU”*, kama kuna kwa njia inamaanisha kuna njia.
Kwa hiyo tazama kuna njia ya imani katika DAMU YA YESU unayotakiwa kuitumia. Kwa hiyo unaweza ondoa neno *njia* na ukaweka *mkakati* sababu kama ni kwa mkakati ina maanisha kuna mkakati. Hivyo itasomeka hivi _“kwa mkakati wa imani katika damu yake”_
Kwa hiyo kama unaenda vizuri kidarasa unatafuta kujua kwanza huo mkakati kabla ya kutembea kwanza kwenye huo mkakati.
Maandiko yanasema NENO ni Nuru, na taa miguu pangu. MUNGU hakuongozi tu kwenye njia bali anakuongoza na hatua zako, kwa hiyo huwezi sema unatembea tu kwenye njia bila hatua,maana hatu aza mwenye haki zinaongozwa na BWANA. Biblia inasema neno lake ni taa na nuru miguuni petu yaani ni mwanga wa njia, maana yake inakulazimu kutazama vizuri mkakati.
Kama uko jeshini au kama unatazama sinema za vita, yaani utajua kuwa hakuna kiongozi anaruhusu watu wake kutumia mkakati wasio ujua kabla, kwa hiyo wale viongozi wa kikundi vidogo vidogo na mkakati ulioko, sasa afande anaona mkakati sasa wewe unaweza ukawa unatazama sehemu yako tu lakini kiongozi anaona Askari wa kawaida, askari wa mizinga, hawa wa ndege n.k Wote anawatazama kwa pamoja, wewe ni askari wa mguu unataka kujitazama kivyako ila haiendi namna hiyo. unaweza ukasema Damu ya Yesu ni silaha na unapozungumzia, silaha ina maana unataja vita yaani uwanja wa mapambano kwa hiyo lazima utazame katika upana wake.
Sasa maandiko yanasema “kwa njia ya imani katika damu yake, ili aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa *Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa*; *apate kuonyesha haki yake wakati huu*,[sasa hapa ni dhambi zilitangulia kufanywa na zinaleta shida wakati huu]. ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu”. Kwa hiyo anataka mkakati wa Damu yake ufanye kazi ili aoneshe haki yake kwamba anaweza akashughulikia dhambi zilizotangulia kufanywa ili aoneshe haki yake wakati huu.
Sasa ukisoma *Yakobo 2:20*
_Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?_ [maana yake imani inatakiwa izae na ili iweze kuzaa inahitaji uhai].
*Yakobo 2:26* inatupa kujua kuwa Imani pasipo matendo imekufa, kwa hiyo ukitaka kupima imani pima matokeo sio mistari jinsi ilivyo. Imani inaletwa kwako ili izae na sio pambo kama yalivyo mapambo mengine. Imani inatakiwa ikuletee matokeo yaliyofanya imani yako. maana *Warumi 10:17* inasema _“Basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo”_ kwa hiyo hilo neno lililokufanya ukasikia linatakiwa likupe matokeo.
Sasa kama imani yako iko hai inafanya kazi tutaangalia matokeo yaani matunda maana mistari uliyoshika haikusaidii.
Sasa sikuambii kuwa na mistari mingi ya biblia ni vibaya niulize mimi nitakusimulia, najitahidi kusoma biblia kila mwaka na nimalize na ili nisichoke kila mwaka nanunua biblia Mpya, kwa hiyo nasoma mwanzo mpaka ufunuo, kwa sababu kusikia huja kwa neno la Kristo. Kwa hiyo kama nimesoma 20% ya biblia ina maana nitasikia kwa 20% kitu Mungu anasema, ksa hiyo ili kusikia zaidi inabid niongeze kusoma neno la Mungu.
Maana kusikia hakuji kwa kuomba, bali huja kwa kusikia neno, kwa hiyo kama huna neno unaweza msikia Mungu akisema ila usisikie anachosema.
Ndivyo biblia inasema unaweza ukasikia, na usielewe kwa hiyo kama nataka kumsikia kwa wigo mpana Mungu inatakiwa nijaze neno la Bwana ndani na sio nijaze tu neno bali, nilisaidie kile ambacho Mungu anataka nipate, na ndani yake inatengeneza imani.
Kwa hiyo ninapoona eneo fulani ndani yangu halina matokeo ya kibiblia, kwa lugha nyepesi ni kuwa imani uliyonayo imekufa. Usijaribu kujihesabia haki, imani yako haina matendo, shetani nae imani anayo kwa hiyo msitishane. Kwa hiyo ninachosikia rohoni, ni kwamba uweze kuimarisha imani yako kimatendo juu ya DAMU YA YESU wewe mwenyewe.
Nilipoamka leo nilikaa na nikamweleza mke wangu na nikamwambia kuwa leo ni siku ya ajabu sana akaniuliza kwanini nilimwambia ni kama hii semina iliisha jana, akaniuliza kwanini nikamwambia leo sina kitu cha kusema maana Mungu hajanipa cha kusema kwa sababu kuna semina naweza ona mapema, mfano naweza jua kuwa semina ya mbeya itakuwa nini kwa siku tatu au nikajua semina ya mwaka ujao.
Sasa ya leo sikuona kitu, kwa hiyo mke wangu akasema huenda tumeongeza siku ambazo Mungu hakutaka tuweke nikasema semina ya leo iko ila sijui Kwanini Mungu kanyamaza, na nikasema redio yangu huku ndani iko wazi, akisema saa hiyo hiyo nitasikia. Basi baada ya masaa mawili Mungu alinisemesha na kasisitiza hiki ninachokuambia. *kuwa na imani binafsi ya kimatendo juu ya Damu ya Yesu*.
*Waebrania 11:28*
_Kwa imani akaifanya Pasaka, na kule kunyunyiza damu, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao._
*1 Wakorintho 5:7*
_Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;_
Kwa hiyo agano la kale walikuwa na Pasaka na agano jipya tuna pasaka. Kwa hiyo hakukuwa na haja ya pasaka leo kama kusingekuwa na unahitaji wa Pasaka wakati huu kama kusingekuwa na tatizo linalohitaji msaada wa mkakati huu, wa Damu ya sadaka iliyoitwa Pasaka.
Tofauti yake ni kwamba matatizo ni yale yale na mkakati ni ule ule, ila kinachotumika ndani kiko tofauti, walitumia damu ya kondoo ila sasa tunatumia damu ya Yesu.
Kwa hiyo huwezi soma huo mstari wa *1 Wakoritho 5:7* bila kurudi na kutafuta yule Pasaka wa kwanza namna alivyotolewa kwa imani.
Ngoja nikupe faida kadhaa hapa, kama nne hivi ambazo zitakusaidia kupata shauku ili ujenge imani yako kimatendo kutoka katika habari hii ya Musa.
*1. IMANI YAKO HIYO ITAKUSAIDIA IKIWA MUSA WAKO HATAPEWA MAELEZO YA KUPEWA KUTUMIA DAMU YA YESU KWA NIABA YAKO*.
Ukisoma *Waebrania 11:28* bila kuangalia ilipotoka utafikiri Musa alichinja pasaka kwa niaba ya wengine wote angalia _“Kwa imani akaifanya Pasaka, *na kule kunyunyiza damu*, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wao”._
Ilivyoandikwa unaweza ukafikiri Musa alitoa kwa niaba yao, ila haiko hivyo angalia;
*Kutoka 12:1-4,7*
_BWANA akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia, Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu. Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja; na ikiwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana-kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na watwae mwana-kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwana-kondoo. *Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla.*_
Angalia vizuri ule mstari wa tatu _“Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi *huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo*, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja”_
Kwa hiyo kama mko watano, ina maana mwana kondoo mmoja, kwanini alisema kila mtu, kwa tafsiri ya kawaida kila mtu maana yake aende kwenye zizi na achukue kondoo wake. Kwa hiyo baba achukue mama achukue na mtoto achukue.
Lakini ukisoma biblia vizuri inasema mwanakondoo mmoja na watu walioko kule ndani. Lakini alipokuwa anasema kila mmoja maana yake nini?
Mungu alikuwa anazungumza nao kuwaonesha umuhimu wa kuwa na imani binafsi kila mmoja, kwa hiyo haijalishi ni nani anaenda kuchukua mwana kondoo kiimani kila mmoja ndani ya familia ahusike kwenda kuchukua mwana kondoo.
Biblia inazungumza mstari wa saba juu ya application yake anasema _*“Nao watatwaa [sasa kama mko saba ndani ya nyumba mtatwaa ile damu na kupaka kwenye miimo ya milango na kizingiti cha juu kila mmoja lazima ashiriki], baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla.”*_
Kwa *hiyo kama* kumi ina maana mtashikilia kila mmoja kupaka hapo. Huyu ni Mungu anazungumza na Musa na alisema kila mmoja atatwaa. Sasa angeweza kusema kiongozi wao ndio atwae. Lakini alipokuwa anaweka watu wote wahusikie alikuwa anazungumza juu ya imani yao maana wasomaji wa Biblia wanajua kabisa, imani ni mkono ina maana unapomsindikiza mwenzako kwa imani ina maana unaenda pamoja nae, alipo upo, anachofanya na wewe unafanya.
Kwanini nimekueleza jambo hili kwa sababu huoni Mungu akimuambia Musa nenda kachukue kondoo alafu chinja kwa ajili ya kila nyumba, huoni maelekezo hayo. Na inahitaji nidhamu sana kwa mtumishi kuweza kuwaeleza mambo hayo kwa sababu wameona namna Farao alivyosumbua na hawakuona usumbufu wake kwa sababu Musa na Haruni ndio walimuona Mungu wakiwa wawili hawa wengine wako nyumbani kwao wanaendelea na shughuli zingine. Yeye peke yake ndio alikuwa anapambana na Farao na kushughulika na Mungu.
Sasa inapofika katika lile pigo la Mwisho, Haruhusiwi kufanya kwa niaba yao anataka kila mtu, sasa wewe fikiri ndio unataka akufanyie. Unaweza shangaa unamkuta Musa wa kwako ili akusaidie na anakuambia Mungu hakunipa maelekezo. Sasa unahitaji nidhamu kali ya kumtii Mungu kuliko kufuata cha watu.
Hapo watumishi wengi sana tunakwama, kwa sababu tunawaogopa watu kwa hiyo tunafanya vitu vingine ambavyo Mungu hakusema. Kama Musa wako hakupewa maelezo ya kutumia Damu kwa niaba yako, saa nyingine Musa wako atapewa, *saa nyingine kama hajapewa nani atakusaidia kama huna imani yako binafsi?.*
*2. IMANI YAKO BINAFSI ITAKUSAIDIA WAKATI MUSA WAKO AMEKOSA NAFASI YA KUKUSAIDIA WAKATI AKIWA NA MAJUKUMU MENGINE WAKATI UNAMHITAJI*
*Kutoka 12:21-23*
_Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni, mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo mkamchinje pasaka. Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi. Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, BWANA atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi._
Musa alisema maneno magumu kidogo kuwa kila nyumba wakipaka damu hawaruhusiwi kutoka kama wanataka msaada, ile damu ilikuwa inashughulika na kitu gani? *Warumi 3: 23-25* ule wa 23 unasema _“wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Pia anazungumza juu ya Damu na pia anazungumza juu ya imani.”_
Kwa hiyo kuna dhambi zilizotangulia kufanywa zinazowakwamisha watu katika maisha yao. Wana wa Israel katika kipindi kile cha Musa, walikuwa wanashughulika na urithi mbaya uliotokana na watoto wa Mzee Yakobo. Yakobo hakuwa na shida kwa watoto wake ila watoto wake ndio walileta shida walipomuuza mwenzao.
Mungu alimwambia Ibrahimu, kuwa watoto wako watakuwa watumwa katika nchi isiyokuwa yao. Na tunajua kuwa walienda Misri kwa sababu ya njaa. Sasa hawa wengine walifanya dhambi walipomuuza mwenzao kwa jinsi ya kiroho walimuua kwa maana walitangaza mauti mpaka kwa baba yao na mama yao na wakalia msiba.
Kwa hiyo waliua na dhambi iliingia hapo na ile dhambi iliwatesa sana na ile dhambi ndio iliwafanya wakae pale mpaka wakawa watumwa baada Yusufu kufa. Sasa saa ya kutoka hawawezi kutoka mpaka wameshughulikia ile dhambi pale na kasome biblia yako katika agano La kale ilikuwa ni jino kwa jino kwa hiyo damu ikimwagika inasafishwa na Damu nyingine.
Sasa Mungu hakutaka kuua wazaliwa wao wa kwanza aliamua kumtoa kondoo kwa niaba yao ili kushughulika na dhambi ya kurithi na urithi mbaya unaowatesa, kwa hiyo hawawezi kutoka bila sheria kwa hiyo lazima atumie sheria kabla hajakuonesha haki yako wakati huu lazima ashughulike na kinachokukwamisha wakati huu usipate haki yako.
Kwa hiyo haijalishi dhambi zimetangulia miaka 400, zinaweza shikilia kizazi miaka na miaka kama hujui namna ya kutoka. Nimekueleza kitu cha namna hii ili ujue kuwa Musa alitangaza kwamba kila familia itafute kila mwanakondoo wamachinje na wapake ila Damu kwenye miimo ya malango na kizingiti cha juu.
Sasa yale maneno yalikuwa yanamhusu na yeye pia kwa sababu alikuwa anatangaza kutoka wakati na yeye na mke wake wako Misri, kwa sababu hawawezi kutoka kwa sababu ni watumishi bali ni kwa sababu wameiheshimu Damu ya Pasaka. maana haiwezekani waihubiri Damu ya Pasaka alafu wao wanafikiri watatoka kwa mkakati mwingine.
Sasa huwezi kuhubiri mkakati wa kutoka kwa kutumia Damu na wewe ukasema aaa mimi ni mtumishi wa Mungu nitatoka kwa mkakati mwingine. Hakuna njia ya staili hiyo, kwa hiyo Musa alikuwa anawaambia kama kungekuwa na simu kama leo mimi nafikiri angezima maana wengine wangekuwa wanampigia ili kumuuliza kuwa ivi ulisema kuwa tunamchinja saa ngapi, na wengine wangesema ivi unasema anaefanya kazi ya kuchinja ni baba au mama. Tunapochinja je tunafanya sala yoyote au je watoto wa kike na wakiume wanaruhusiwa kwenda kumwaga Damu? mara simu nyingine inapigwa ili kuuliza hiki na kile.
Ni rahisi sana kusoma yale maneno na ukafikiri kilikuwa ni kitu chepesi kwa hiyo nae Musa kama anataka kutoka hana namna nyingine ambavyo akiweka ile damu na akatoka ina maana atapigwa yeye mwenyewe kwa sababu kavunja sheria na familia yake haitapona. Haponi kwa sababu yeye ni mtumishi wa Mungu bali ni kwa sababu ametumia maandiko yale yale aliyoambiwa ahubiri na ile ile Damu ndio atakayoitumia.
Kwani hatuhubiri kwa sababu hatuna shida au sisi ni wasafi kuliko wengine mtu asikudanganye kuwa kwa sababu eti ni mhubiri yeye hana shida, maana hamna mtu anapeleka application kwa Mungu kuwa tufanye kazi anachagua kwa neema yake, kwa kusudi lake na kutaka kwake si kwa sababu ni wasafi ila ni kwa sababu anataka. kasome biblia yako inasema aliwachagua wanafunzi wake kama alivyotaka mwenyewe
Ndio maana hutaenda mbinguni kwa sababu ya cheti cha utumishi Lazima Damu ya Yesu ifanye kazi. Kama unafikrii natania kasome biblia yako maana Yesu atasema haloo ondoka hapa wewe utendae maovu maana sikuji wewe. utasema pole pole Yesu mbona nilikuwa natoa unabii na nilikuwa nakemea pepo na linatoka.
Sasa kwanini unasema hunijui wakati yote ulikuwa unatenda, atasema ni kwa sababu ya neno langu na jina langu ndio nilikuwa natenda. Ndio maana ninakuambia imani yako itakusaidia wakati Musa wako nae yupo nyumbani kwake na anaomba na kutoka nae kivyake.
Saa hiyo sio wakati tena wa kumpigia simu kusema naomba unisaidie wakati na atawajibu kuwa maneno yale niliyowambia yamenifunga na mimi na sina namna ya kutoka.
Ngoja nikupe mfano huu;
*USHUHUDA*
```Kuna dada mmoja alikaa kwa mume wake na alikuwa anapata mimba na zinaharibika na ziliharibika karibu mimba kama sita hivi. tulikuwa mahali fulani kwenye nyumba fulani alitusikia pale na kesho yake ofisini tuliletewa barua 7 full scale,anajieleza. Akajieleza matatizo yake na akasema kama Mungu akiwapa kibali mnisaidie. Basi tulijadaliana na mke wangu baada ya kuomba na tukamtafuta akaja tuliongea na tukamtia moyo vizuri kabisa na baada ya muda alipata ujauzito na tulimpa na mistari. Baada ya miezi miwili akaja tena ofisini akaniambia kuwa mimba imetoka. nikamuuliza swali kwanini umetoa mimba? akasema nimeenda chooni imetoka yenyewe. nikajua hakuelewa swali langu.
Nikamuuliza umewahi kuona maiti inapata mimba? akasema hapana nikamuuliza tena je, kinachopata mimba ni mwili au roho?. nikamuuliza kuwa kama mwili usipokuwa na roho haupati mimba je kinachopata mimba ni roho au mwili.? akanitazama akasema ni roho.
nikamwambia mwili kazi yake ni kutengeneza mwili, kwa hiyo nikamwambia kama roho yako ndio inayopokea ujauzito na kukabidhi kwa mwili ili kutengeneza mwili.
sasa nikamuambia kwa hiyo mwenye mamlaka ya mwisho ya kupata mimba sio mwili ni roho. kwa hiyo nikampeleka kwenye maandiko. na kumsemesha mtoto kukaa tumboni kuwa haruhusiwi kutoka kabla ya miezi tisa. Na nilimpa na mistari na nilimfundisha tena kitu cha kufanya.
Baada ya muda tena alipata mimba na tukasema tutazidi kukuombea. sasa baada ya miezi miwili akaanza kuona Dalili za kutoka kwa mimba tena, na alitutafuta ofisini na kila mahali na alitukosa.(Tulikuwa eneo lile lile pale pale mjini)
Alitutafuta kila mahali hakutupata, basi akarudi nyumbani kwake amenyong’onyea. sasa alipofika kwake Roho Mtakatifu alimkumbusha ile mistari niliyompa. na yule mama akaanza kufuatilia ile mistari tuliyompa wakati ule na ghafla ile haja ya kuwa na imani yake peke yake ikaongezeka. Sasa unapozungukwa na watu wanao kusaidia kukuombea na itafika kipindi, unapotafuta mpenyo na sisemi kuombewa ni vibaya. sasa itafika mahali unataka kupiga simu na kwa kuwa unakuwa kwenye mahangaiko unaweza kuta hata simu hukuchaji vizuri na inazima.``` Hapo unakuwa huna mtu tena wa kukusaidia na *ndio maana kuwa na imani yako mwenyewe ni muhimu.*
Kwa sababu hiyo Mungu alimwambia Musa kuwa, lazima kila mtu aende zizini, ndio maana nasema ukisoma Waebrania 11 utafikiri ni Musa aliwafanyia ila ukisoma katika Kutoka unaona jinsi ambavyo Mungu alikuwa anasisitiza umuhimu wa kuwa na imani binafsi juu ya Damu ili kila mmoja kule ndani aweze kufanya peke yake. Maana kuna kipindi unaweza kuwa na akina Musa wengi sasa si vibaya maana watakusaidia kuomba. Ila kuna kipindi, imani yako inakuwa chini kiasi ambacho huna hata msaada tena na hapo ndipo umuhimu wa kuwa na imani binafsi unaongezeka. Biblia inasema nitafuatia mfalme akiwa amechoka maana ndio saa ambayo unakuwa huwezi hata kufanya lolote. na *ndio maana ni muhimu kuwa na imani yako hata kama ni kidogo*.
*3. IMANI YAKO HIYO ITAKUSAIDIA WEWE NA FAMILIA YAKO WAKATI WATU WANAOKUHUSU WAMEAMUA KUTOKUAMINI MANENO YA MUSA JUU YA DAMU*
Wana wa Israel najua katikati yao walikuwepo wabishi yaani watu ambao hawakuamini. maana kuna namna ubishano ulikuwepo kwa mfano Musa alipooa mwanamke Mkushi kuna wengine walibisha, kuwa haiwezekani Mungu aseme na Musa peke yake. na najua pia kuna wengine walikuwa hawaoni kwao kwa sababu kwao kulikuwa na mwanga ila kwa wengine ilikuwa giza. Musa na Haruni kila walichoambiwa na Mungu hawakubisha maana waliona Mungu akitenda.
Naamini walikuwepo waliosema haiwezekani Bwana hii damu ya kondoo ndio tuitumie hivyo, labda wangetuambia kuwa tupake juu ya wazaliwa wa kwanza ni sawa ila, hii ya kutuambia hii *DAMU YA KONDOO NDIO IWE DAMU YA PASAKA*, alafu tupake kwenye milango na kizingiti cha juu wazaliwa wa kwanza watapona.
Lazima kuna watu walisema sisi ni uzao wa Ibrahimu hatuwezi kukutana na shida ya namna hii na kumbuka pia kuna wapendwa nao wanasema aaah mimi nimeokoka siwezi kutana na shida ya namna hii, na wanaacha DAMU pembeni. Kumbuka hawa Wayahudi kuna siku moja walibishana na Yesu na kusema sisi ni uzao wa Ibrahimu hatujawahi kuwa watumwa wa dhambi hata siku moja walikuwa wabishi na ndio maana Mungu aliwaita wenye shingo ngumu. kwa hiyo imani yako ni muhimu sana ili kuweza kushinda ubishi wa namna hii.
Ni sawa sawa na watu ambao wanabisha kuokoka na siku wakikutana na Yesu ndipo watakukumbuka au wakienda ule upande wa Pili ambao alienda yule tajiri wakati wa Yesu alipotoa mfano wa Lazaro ndipo watakumbuka umuhimu wa Mpendwa wao aliyekuwa anawashuhudia habari za Mungu.
*4. IMANI YAKO HIYO ITAKUSAIDIA WEWE NA FAMILIA YAKO WAKATI MNAEMTEGEMEA KIIMANI ANAPOKUWA MZITO KUWAONGOZA KATIKA NJIA YA DAMU YA YESU*
Musa alimtegemea Haruni ila ndiye aliye waongoza watu kuabudu ndama. Ile kwamba wote mmeamka mna Yesu haina maana ikifika jioni wote mna Yesu. huwezi jua kitu kinachopita hapo mchana.
Na unakuta ni mtu mlikuwa mnaemtegemea sana kiimani na mnamkuta anakuja na ndama nyumbani mnamuuliza je huyu wa kuchinja au, anasema hapana ni wa kuabudu mnamuuliza imetoka wapi anasema mafunuo haya Bwana nimeonana na Mungu kwenye maombi.[ndio maana ni hatari kuwa na maombi bila neno, maombi yanaendana na neno].
Unaweza kuta mtu anasema ili akusaidie anasema leta sadaka kwanza, maana sadaka haiwezi kununua kitu kutoka katika kitu cha msalabani. Najua sehemu ya sadaka na umuhimu wa sadaka na hutoi sadaka kwa sheria bali unatoa kwa imani. kwa hiyo mtu asikulazimishe kutoa sadaka bali toa kwa imani.
Je kama mtu mnayemtegemea hayupo mtafanyaje? ndio maana lazima awepo mwingine, na ndio maana neno la Mungu halifungwi yaani mkimuua Yakobo, jua kuwa Petro yuko. Na mkimuua Petro mwingine atasimama.
Kwa hiyo jenga imani yako ndani ya damu ya Yesu maana kila aliyeokoka ana kazi na anaweza tumia Damu ya Yesu. Biblia inasema iweni hodari katika Bwana katika nguvu zake. Kwa hiyo iweni hodari na vaeni silaha zote. Huwezi kuwa Hodari kama hufanyii mazoezi ulichosoma
Ndio kama Kocha wa mpira anataka mtu hata kama ni mzuri sana anaweza kupiga chenga sana na kucheza vizuri, lazima afanye mazoezi ili ajue namna ya kucheza kiteam na kuwapasia wenzake ili kila mtu aweze kuwa na uwezo wa kufunga goli na adui ashindwe amkabe yupi. Maana hata goalkeeper anafundishwa namna ya kufuga goli.
Kwa hiyo chukua ile *Waebrania 9:16-17*, maana palipo na agano la urithi lazima kuwepo na mauti na wewe chukua mauti ya Yesu maana inapangua mauti zingine. Kwa hiyo chukua haya maneno tafakari na chukua hili maana hata mimi kabla sijaleta hapa lazima nione kinafanya kazi.
Huwezi kushugulikia masuala ya urithi mbaya kama hujaokoka maana Damu ya Yesu ni damu ya agano na sio kila mtu na unaingia kwenye agano kwa kuokoka ili uwe na haki. Hawezi kukuonesha haki yake kama Damu haijamwagika mahali.
ooh.. Funika macho yako… Kama hujaokoka hakikisha unaokoka na kumpokea Yesu awe Bwana wa maisha yako..
🎶🎶wimbo wa _*Ni Salama Roho moyoni Mwangu.🎶*_🎶
Baada ya hapo bonyeza link pale juu kusikiliza maombi ya kuokoka na baraka. Pia kuna namba za sadaka ziko pale kama utasukumwa na Roho Mtakatifu kutoa au kumshukuru Mungu kwa neema hii ya kupata masomo haya kwa siku zote nane.
*Tuonane tena semina ijayo Njombe kuanzia Alhamisi 19-22 OCT 2017*. *Ubarikiwe sana na Yesu 🙏🙏🙏*
Huduma Ya Mana Tanzania na Mwalimu Christopher Mwakasege
mwakasege.org

Friday, 15 September 2017

MWONGOZO WA KUTAFAKARI NA KUOMBEA NDOTO ZENYE UZINIFU AU UASHERATI NDANI YAKE Na Mwl. Christopher Mwakasege.




Bwana Yesu asifiwe sana!
Leo nataka tujifunze juu ya “Mwongozo wa kutafakari na kuombea ndoto zenye UZINIFU AU UASHERATI ndani yake”.
Maneno haya ‘uzinifu na uasherati’ yanahusu ufanyikaji wa tendo la ndoa usio halali kibiblia. Uzinifu linatumika zaidi wakati tendo la ndoa limefanywa na mtu ambaye hajaoa au hajaolewa. ‘Uasherati’ linatumika zaidi wakati tendo la ndoa limefanywa nje ya ndoa na mtu ambaye ameoa au ameolewa.
Mtu anayepata ndoto zenye mambo hayo, huwa zina madhara makubwa sana ya kiroho, na ya kimwili – kwa aliyeota ndoto hizo!
Kumbuka kwamba: Neno la Mungu la biblia, kwa kushirikiana na Roho Mtakatifu, linatuongoza kujua namna ya kutafsiri na kuziombea ndoto za aina yo yote – ambazo ni pamoja na hizi zenye mambo ya uzinifu au uasherati ndani yake.
Ni muhimu kwako kupata nafasi ya kusoma, na kutafakari mistari ya biblia, ambayo nimeambatanisha na somo la leo. Hebu tujifunze somo la leo kwa mtiririko ufuatao:
(1) Ukiota unazini kwenye ndoto maana yake nini? Ina maana ya kwamba
(a) Umeunganishwa kiagano na roho ya (au pepo la) uzinifu au uasherati – kufuatana na aina ya mtu uliyekuwa unazini naye.
Neno linasema…
“Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.”
~1 Wakorintho 6:16,17.
(b) Unapoteza uwezo wa kufaidi matunda ya ufalme wa mbinguni.
Neno linasema…
“ Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, 10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.”
~ 1 Wakorintho 6:9
(c) Ni ishara ya kwamba mwili wako umepandikizwa mbegu ya kukuzuia usiweze kuomba, au usiwe mwombaji.
Neno linasema…
“ 18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”
~ 1 Wakorintho 6:18 – 20.
(d) Umepandikizwa roho na mbegu ya kumwasi Mungu tunayemwabudu katika Yesu Kristo.
Neno linasema…
“10 Hivyo Edomu wakaasi chini ya mkono wa Yuda, hata leo; wakaasi na Libna zamani zizo hizo chini ya mkono wake: kwa sababu alikuwa amemwacha Bwana, Mungu wa baba zake. 11 Tena ndiye aliyefanya mahali pa juu milimani pa Yuda, na kuwaendesha katika uasherati wenyeji wa Yerusalemu, na kuwakosesha Yuda.”
~ 2 Mambo ya Nyakati 21:11
Na Pia neno linasema…
“Tena umezini na Wamisri, jirani zako, wakuu wa mwili; ukaongeza mambo yako ya kikahaba, ili kunikasirisha.
~ Ezekiel 16:26
(e) Ni njia ya kupanda ‘mbegu’ ya uzinzi, au ya uasherati, ambayo isipoondolewa kwa damu ya Yesu, itachipuka katika maisha ya baadaye ya mtu aliyeota hiyo ndoto.
Neno linasema…
“18 Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi. 19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;”
~Mathayo 15:18, 19
Pia katika Mathayo 5:27, 28
Neno linasema...
“27 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; 28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”
~ Mathayo 5:27, 28
(2) Ukiota unazini kwenye ndoto na ndugu yako wa karibu – kama baba au mama mzazi, au dada yako, au kaka yako, au mkwe, au mjomba au mke wa mjomba….ina maana ya kwamba:
(a) Unaandamwa na roho ya kukataliwa na kutengwa na wale wa imani moja na wewe kiroho!
Neno linasema…
“1 Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye. 2 Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo. 3 Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo. 4 Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu; 5 kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.”
~ 1 Wakorintho 5:1 – 5.
(b) Utasumbuliwa na magonjwa au hatari zingine kwenye mwili wako kwa lengo la kukuua. Soma 1 Wakorintho 5:1 – 5.
(c) Unaandamwa na roho ya mauti.
Neno linasema…
“11 Na mtu mume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao. 12 Na mtu mume akilala na mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauawa; wamefanya yaliyo uchafuko; damu yao itakuwa juu yao. 13 Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao. 14 Tena mtu mume akimwoa mke pamoja na mama yake, ni uovu mkuu; watachomwa moto, yeye mume na hao wanawake pia; ili kwamba usiwe uovu kati yenu.”
~ Walawi 20:11 – 14.
(d) Unaandamwa na roho ya kurithi iliyobeba uovu.
Neno linasema…
“17 Tena mtu mume akimwoa umbu lake, binti ya baba yake, au binti ya mama yake, na kuuona utupu wake, na huyo mwanamke kauona utupu wake huyo mume; ni jambo la aibu; watakatiliwa mbali mbele ya macho ya wana wa watu wao; amefunua utupu wa umbu lake; naye atauchukua uovu wake… 19 Usifunue utupu wa umbu la mama yako, wala umbu la baba yako; kwa kuwa huyo amefunua utupu wa jamaa yake ya karibu; watauchukua uovu wao. 20 Tena mtu mume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake; watauchukua uovu wao; watakufa bila kuzaa mwana.”
~Mambo ya Walawi 20:17, 19, 20.
(e) Utasumbuliwa na tatizo la kutokuzaa watoto.
“20 Tena mtu mume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake; watauchukua uovu wao; watakufa bila kuzaa mwana. 21 Tena mtu mume akimtwaa mke wa nduguye, ni uchafu; ameufunua utupu wa nduguye; hao watakuwa hawana wana.”
~Mambo ya Walawi 20: 20, 21.
(f) Unafungulia roho ya ukahaba.
Neno linasema…
“Usimnajisi binti yako, ili kumfanya awe kahaba; isiwe hiyo nchi kuuandama ukahaba, na nchi kujawa na uovu mkuu.”
~Mambo ya Walawi 19:29
(g) Umepandikizwa au unapandikizwa roho au pepo la kukataliwa na waliookoka (Ikiwa uliyeota ndoto hiyo umeokoka); au wakristo wanaokufahamu.
Neno linasema…
“9 Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi. 10 Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. 11 Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye. 12 Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani? 13 Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu. Ninyi mwondoeni yule mbaya miongoni mwenu.”
~1 Wakorintho 5:9 – 13
(3) Ukiota ndoto unazini au unafanya uasherati na mtu wa “imani” nyingine maana yake nini? Ndoto ya namna hii ina maana ya kuwa kuna roho au pepo lililoingia nafsini mwako ili.
(a) Kuua na kuharibu imani yako ili uiache na ufuate imani nyingine ya huyo uliyezini naye kwenye ndoto.
Neno Linasema…
“15 Usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi, watu wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, na kuitolea sadaka miungu yao; mtu mmoja akakuita, ukaila sadaka yake. 16 Ukawaoza wana wako binti zao, nao binti zao wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, wakawavuta wana wenu wafanye uzinzi na miungu yao.”
~Kutoka 34:15, 16
Pia Neno linasema…
“1 Bwana, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang'oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe; 2 wakati Bwana, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao; 3 binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake. 4 Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi.”
~Kumbukumbu ya Torati 7:1 – 4
Pia Neno linasema…
“1 Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu; 2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao.”
~ Hesabu 25:1,2
Pia Neno linasema…
“1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, 2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda. 3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo. 4 Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake. 5 Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni… 7 Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni. 8 Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu. 9 Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili,”
~1 Wafalme 11:1 – 5, 7 – 9.
(b) Kukufanya urudi nyuma kiroho, na usiweze kumfuata vizuri Mungu unayemwabudu katika Kristo Yesu.
“1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, 2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda… 6 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.”
~1Wafalme 11:1, 2, 6.
(c) Inafungua mlango wa maadui kuinuka juu yako na dhidi yako, na kupata nafasi ya kukusumbua na kukufanya ukose utulivu.
“1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, 2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda…14 Ndipo Bwana akamwondokeshea Sulemani adui, Hadadi Mwedomi; yeye alikuwa wa wazao wake mfalme wa Edomu…23 Tena, Mungu akamwondokeshea adui mwingine, Rezoni mwana wa Eliada, aliyemkimbia bwana wake Hadadezeri mfalme wa Soba.”
~1 Wafalme 11:1, 2, 14, 23.
(d) Inafungulia pepo la mauti likiwa na lengo la kukua, kwa nia ya kujitafutia sifa kwa ‘mungu’ wake.
Neno linasema…
“1 Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu; 2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. 3 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli. 4 Kisha Bwana akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa hao watu, ukamtungikie Bwana watu hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali za Bwana ziwaondokee Israeli. 5 Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha na Baal-peori. 6 Na tazama, mtu mmoja miongoni mwa wana wa Israeli akaja na kuwaletea nduguze mwanamke Mmidiani mbele ya macho ya Musa, na mbele ya macho ya mkutano wote wa wana wa Israeli, hapo walipokuwa walia mbele ya mlango wa hema ya kukutania. 7 Naye Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, alipoona jambo hilo, akaondoka hapo katikati ya mkutano, akashika fumo mkononi mwake; 8 akamwandama huyo mtu wa Israeli na kuingia ndani ya hema nyuma yake, naye akawachoma wote wawili kwa fumo lake, yule mume wa Israeli na huyo mwanamke kati ya tumbo lake. Basi pigo likazuiwa kwao wana wa Israeli. 9 Nao waliokufa kwa hilo pigo walikuwa watu elfu ishirini na nne hesabu yao. 10 Kisha Bwana akanena na Musa, akamwambia, 11 Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, amezigeuza hasira zangu zisiwe juu ya wana Wa Israeli, kwa kuwa alikuwa na wivu kati yao kwa wivu wangu mimi, hata nisiwaangamize wana wa Israeli katika wivu wangu. 12 Basi kwa hiyo, sema, Tazama, nampa yeye agano langu la amani; 13 tena kwake yeye, na kizazi chake baada yake, litakuwa agano la ukuhani wa milele; kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya Mungu wake, na kuwafanyia upatanisho wana wa Israeli.”
~Hesabu 25:1 – 13.
(e) Inafungulia roho ya wivu
(Kutoka 34:14 – 16 na Hesabu 25:1, 2, 10, 13)
Na roho hiyo inayozaa ugomvi wenye kisasi mara kwa mara
“Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.”
~Yakobo 3:16
(4) Ukiota ndoto unazini na mnyama – ina maana gani? Kwa mfano – kuna mama mmoja aliniandikia kuwa aliota yuko uchi kwenye banda la ng’ombe, na ng’ombe dume akazini naye! Alipoamka toka usingizini alisikitika sana!
Ukiota ndoto za kuzini na mnyama maana yake ni hii:
(a) Umevamiwa na unaandamwa na roho ya mauti,
Neno linasema…
“19 Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa.”
~Kutoka 22:19
Pia Neno linasema…
“15 Tena mtu mume akilala na mnyama, hakika atauawa; nanyi mtamwua huyo mnyama. 16 Tena mwanamke akimkaribia mnyama ye yote, na kulala pamoja naye, mtamwua huyo mwanamke, na mnyama pia; hakika watauawa; damu yao itakuwa ni juu yao.”
~Mambo ya Walawi 20:15,16.
(b) Umechafuliwa kiroho ili uwepo wa Mungu ukae mbali na wewe.
Neno linasema…
“23 Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko”
~Mambo ya Walawi 18:23
(c) Unapandikizwa laana.
“21 Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina.”
~Kumbukumbu ya Torati 27:21.
(5) Madhara ya ziada yanayoweza kumpata MWANAUME akiota ndoto anazini au anafanya uasherati ni pamoja na:
(a) Kupata tatizo la kutoweza kutumia akili vizuri (Mithali 6:32, 33), katika kufikiri kimaisha!
Neno linasema…
“32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. 33 Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.”
~ Mithali 6:32, 33
(b) Maendeleo yake kiroho na kimaisha na kifikra yanakwama kwa kuwa nafsi yake ‘inanaswa’
Neno linasema…
“26 Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani”
~Mithali 6:26.
Nafsi yake iliponasia ndipo panapoweka kipimo cha maendeleo yake
Neno linasema…
“ Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.”
~3 Yohana 1:2.
(c) Nguvu za kiume za uzazi zinapungua au zinapotea kabisa
“3 Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; 4 Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili. 5 Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; 6 Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari. 7 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. 8 Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. 9 Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako; 10 Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni;”
~Mithali 5:3 – 10
(6) Madhara ya ziada yanayoweza kumpata MWANAMKE, ikiwa ataota anazini, au anafanya uasherati kwenye ndoto, ni pamoja na pepo kupata nafasi ya kuingia, na kukaa kwenye kizazi chake
“20 Tena mtu mume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake; watauchukua uovu wao; watakufa bila kuzaa mwana. 21 Tena mtu mume akimtwaa mke wa nduguye, ni uchafu; ameufunua utupu wa nduguye; hao watakuwa hawana wana.”
~Mambo ya Walawi 20: 20, 21
Na pia kumletea madhara kama ifuatavyo:
(a) Kuvuruga mzunguko wake wa damu ya mwezi;
(b) Kuweza kuharibu mimba –ikiwa – huyo mwanamke aliyeota ndoto alikuwa mja mzito alipokuwa akiota ndoto hiyo;
(c) Kuvuruga uwezekano wa kupata mimba – ikiwa ameolewa;
(d) Kuharibu viwango vya utendaji kazi wake kama mwanamke akiwa nyumbani kwake;
(e) Kupandikizwa magonjwa kwenye kizazi chake, au/na kwenye damu yake
(7) Ukiota unazini au unafanya uasherati kwenye ndoto wakati umekwisha chumbiwa au umekwisha chumbia; au wakati zimebaki siku chache za kufanyika kwa harusi yako – ujue maana ya ndoto hiyo ni hii:
KWAMBA: Kuna pepo lililopata nafasi kwako, ili kuvuruga mipango yako ya harusi isifanyike; au hata kama utaolewa, au utaoa – hilo pepo litatengeneza mazingira ya wewe kuachika, au kuachana na huyo mwenzi wako!
“16 Mtu akimshawishi mwanamwali, aliyeposwa na mume, na kulala naye, lazima atatoa mahari kwa ajili yake ili awe mkewe.”
~Kutoka 22:16
(8) Ukiota ndoto unazini, au unafanya uasherati na kichaa au mchawi – ujue maana ya ndoto hii ni; KWAMBA: Shetani anapandikiza hila zake kwenye maisha yako, ili kukusababishia ukataliwe na watu wako!
“ 6 Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake.”
~ Mambo ya Walawi 20:6
(9) Ikiwa ‘eneo’ ulilofanyia uzinifu au uasherati kwenye ndoto uliyoota linaeleweka …yaani kama nyumbani, ofisini, jikoni, makaburini, darasani – nakadhalika – ndoto hiyo inakupa ujumbe gani wa ziada?Ndoto kama hii – yenye kukuonyesha uzinifu, au uasherati ulipofanyika, inataka ujue ya kuwa – kiroho eneo hilo ‘limenajisika’, na ‘kuchafuka’, na lisiposafishwa kwa damu ya Yesu mapema, litatoa nafasi kwa mapepo kujitengenezea ‘kituo’ chao!
“ 20 Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye. 21 Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi Bwana. 22 Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. 23 Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko. 24 Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote; 25 na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa. 26 Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu; 27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;) 28 ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu. 29 Kwani mtu awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao. 30 Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba msifanye kabisa desturi hizi zichukizazo mojawapo, zilizotangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”
~Mambo ya Walawi 18:20 – 30
Na pia Neno linasema…
“2 kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake.”
~Ufunuo wa Yohana 19:2
(10) Hatua zifuatazo zitakusaidia katika kupanga mambo ya kuomba juu ya ndoto za namna hii:
(a) Fanya maombi ya Toba kwa ajili ya mlango uliofunguka na ukaota ndoto za namna hii
(b) Vunja kwa damu ya Yesu aina yo yote ya muunganiko wa kiagano, kati ya nafsi yako (uliyeota ndoto) na roho ya kipepo iliyojiunganisha na nafsi yako, kwa kupitia kwenye ndoto hiyo
(c) Kemea kwa jina la Yesu kila aina ya roho ya kipepo iliyokuja kwako kwa kupitia hiyo ndoto;
(d) Haribu kwa damu ya Yesu aina yoyote ya mbegu ya uzinifu, au ya uasherati au ya ukahaba iliyopandikizwa ndani yako kwa njia ya ndoto hiyo
(e) Omba uponyaji wa eneo lo lote lililopata madhara kwenye roho yako, au kwenye nafsi yako, au kwenye mwili wako, au kwenye mahusiano yako na watu wengine, au kwenye mipango yako, nakadhalika
(f) Omba neema ya Mungu ikusaidie kurejesha kwa upya mahusiano yako na Mungu katika Yesu Kristo
(g) Omba utakaso wa damu ya Yesu ufanyike kwenye eneo ambalo kufuatana na ndoto hiyo – uzinifu ulifanyika hapo.
LA KUKUMBUKA: Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kukupanulia wigo wa ufahamu, juu ya eneo lingine linalohusu ndoto za namna hii ambalo sijaligusia hapa. Mungu azidi akubariki.
Amen
Imetolewa toka Fb Page ya Mwalimu Christopher Mwakasege
Na kuongeza maandishi kama yalivyo andikwa kwenye Biblia Mahali aliposema Kasome Nimekuwekea hapa Usome.( reference from The Bible) Pia usiache kwenda kwenye Biblia Yako Kusoma.
Utukufu na Heshima Vina Wewe Mungu Kwa kupitisha Chakula Hiki Kwa Mwl. Christopher Mwakasege. Cha wakati na chenye msaada Mkubwa na Chenye Nguvu ya Ukombozi Ndani yake. Na Kunifikia Mimi Minister : Enoch Joseph na hata kuwafikia wengine wote Wasomao.
Thank You Jesus.
Thank You Dad Mwalimu C.Mwakasege.

Friday, 8 September 2017

Jufunze kuombea Familia Yako kwa kuizungushia/ kuijengea fance ya ulinzi.



Jifunze ya kuwa ni hekima ya kimungu kujenga wigo ili maadui na watu wasio takiwa kuingia katika Nyumba ya Mtu wasiingie. Kujenga ukuta ni hekima ya kumungu ndiyo nataka ujuwe.
Ndiyo maana utaona.
Neno linasema...
" { Mji mpya wa Jerusalem } ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli." Ufunuo 21:12.
Kwahiyo si tuu kujenga ukuta bali ukuta huo uwe na mageti imara na mazuri. Na sio tu yawepo mageti Bali katika kila Geti pawe na malaika/mlinzi atakaye ruhusu nani aingie na nani asiingie.
Watu wanajenga majumba Makubwa katika nyumba zao, lakini maisha yao na katika ulimwengu wa Roho hawana ulinzi kabisa yaani ni kama nyumba isiyo na ulinzi kabisa.
Maadui wa kila namna wanaingia hata pasipo vikwazo.
Ndiyo maana nabii hosea alisema...
" Basi kwa ajili ya hayo{ makumbukumbu mabaya, mashambulizi ya maadui wa nje, na mawakala wa shetani wajao ili kuharibu na kuuwa} angalia, nitaiziba njia yako kwa miiba{ wigo} , nami nitafanya kitalu juu yake, asipate kuyaona mapito yake." Hosea 2:6
Waombaji wote wanajuwa kujenga ukuta na wakijenga ukuta wanaweka na mageti yachuma na getini wanaweka walinzi makini ambao ni malaika wa Mbinguni.
Unaweza ukajiuliza unazungushaje wigo kwenye familia yako. Ni uamuzi wako
Zungushia familia yako na Damu ya Yesu
Na Zungushia familia yako na Moto wa Roho mtakatifu.- " And I will be to her a wall of fire all around, declares the Lord, and I will be the glory in her midst.’' Zachariah 2:5.
Kila mwenyenia ovu akigusa Moto umchome.
Katika Jina la Yesu
Familia yako ilindwe kwa Damu ya Yesu
Familia yako izungushiwe wigo wenye Moto wa Roho Mtakatifu.
Amen.
___________________
Minister: Enoch Joseph
Life word Ministry
©2017.

Malaika




Wako malaika wengi sana na wapo kwenye vitengo tofauti tofauti. Wako malaika wanao deal na uponyaji kiongozi wao ni Malaika Rafael , wapo malaika wa vita kiongozi wao ni Malaika Michael , wako Malaika watoa taarifa toka kwa Mungu wakiongozwa na Malaika Gabriel .
_______________
Na huu ni ujumbe toka kwa Mungu kuja kwako.
Ujumbe Unasema...
" … Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema. Na tazama! Utakuwa bubu, usiweze kusema, mpaka siku ile yatakapotukia hayo, kwa sababu hukuyasadiki maneno yangu; nayo yatatimizwa kwa wakati wake." - Luka 1:19-20
Sujafahamu ni jambo gani umekuwa ukimwomba Mungu akutendee kwa Mzigo na kwamachozi lakini kila baada ya kuomba inakuja hali ya kukata tamaa na kuliona hilo jambo ni kubwa sana.
Sikia neno la Mungu hili ambalo Malaika wa Bwana amekuja kukufikishia ujumbe kwamba jambo hilo litatimia kwa wakati wake.
Kinywa ni chanzo kikuBwa cha kukuzuia usifanikiwe
¶- Usimwambie Mtu kitu Bwana anakwenda kukutendea. Subiri wataona kwa Macho.
¶- usijibu maswali yenye Mtego wa kukukirisha kwa kinywa chako kushindwa..
¶- Usikiri wanacho wanacho kiri walio shindwa bali itazame ahadi ya Bwana kwako.
" Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya."- Kutoka 14:14.
Bwana Mungu akutimizie Mahitaji yako katika Jina la Yesu.
Amen.
______________
Minister: Enoch Joseph
Life word Ministry
©2017

Maamuzi Yako.




My God My God.
Maamuzi yako ya sasa Juu ya nini unafanya na nini usifanye, Juu ya nini Unakipenda na nini hukipendi Yana impact||Matokeo makubwa sasa unapo fanya maamuzi, kesho yako baada ya kufanya Maamuzi, Keshokutwa yako Baada ya kufanya Maamuzi, Kizazi chako cha ~[kwanza- 1] yaani watoto wako na Jamii ya sasa, Kizazi cha ~[Pili -2] yaani kizazi cha pili yaani watoto wa watoto wako{ wajukuu} , Kizazi cha ~[tatu -3 ] yaani watoto wa wajukuu wako, na kizazi cha ~[nne -4] yaani watoto wa watoto wa wajukuu zako.
Haya yanaitwa Maamuzi. Yes ni Maamuzi yako. Unaweza ukawa unafanya maamuzi kwa kucheka au kwa kuchekewa na wengi lakini maamuzi hayo yanaweza kufaidisha vizazi vingi sana toka ulipo au yakaumiza wengi sana kwa sababu yako.
Sijui kama unafahamu yakuwa neno linasema...
"... kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu." Kumb 5:9-10
Nataka uonekitu Mungu huwa anabatiliza uovu wa watu, maamuzi ya uovu wa vizazi vitatu mpaka vinne. Lakini Mungu huwabariki Maelfu kwa Maelfu ya wampendao. Wafanyao maamuzi mazuri.
Adamu na Eva walifanya Maamuzi katika Bustani ya edeni lakini maamuzi ya watu wawili yalisababisha Uwepo wa Mungu uondoke na kufukuzwa Bustani ya edeni, Maamuzi yale yali haribu kabisa uhusiano kati ya Mungu na Mwanadamu. Mimi sijui kama hawakujua au walijuwa ila ninacho fahamu hawakujuwa kwamba Maamuzi yao yalikuwa yanategemewa na Dunia nzima.
Huwa unazingatia haya Unapofanya Maamuzi katika Maamuzi yako. Maamuzi yako hapa duniani yana impact hapa duniani na Mbinguni. Sijui kama unajuwa Yesu aliwaambia watu hili wazi wazi bila vificho.
Yesu alisema...
" Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu." Luka 15:7
Yaani Maamuzi ya Mlevi mmoja, maamuzi ya jambazi mmoja, maamuzi ya malaya mmoja, maamuzi ya Muongo mmoja, maamuzi ya msengenyaji mmoja na my God maamuzi ya Mwenye dhambi mmoja atubuye na kufanya maamuzi ya kumfuata na kumpenda Yesu na kuambatana naye.
Mbinguni shangwe na nderemo na shangwe na furaha hurindima kwaajiri ya maamuzi ya mtu mmoja.
Pengine unaweza usielewe.
Yaani iko ivi
Mungu aliye ziumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo hufurahi.
Malaika maelfu kwa makumi elfu hufurahi.
Na kila aliye Mbinguni hufurahi.
Lakini too bad Maamuzi ya waliookoka 99.. Ambao wametenda dhambi nuruni na sirini ambao wamefanya maamuzi ya kuto kutubu.
Maamuzi juu ya kile Mungu anakusemesha juu ya kazi ya Mungu yana impact kwa watu wa vizazi vingi sana. Inaweza ikawa ni Juu ya
~ Kumwimbia Mungu.
Ukikubari uta wabariki wengi na kuwaleta wengi kwa Yesu.
~ Ku support kazi ya Mungu.
Iwe ni kwa hali na Mali, iwe ni kununua vifaa vya Injiri ya Yesu, iwe ni kwa kuwapelewa watendakazi shambani mwa Bwana field kufundisha neno la Mungu, etc
~Iwe kwa kutii sauti Ya Mungu Juu ya kile anataka ukafanye. Yona aliamua kulakona ahsante Yesu alimbananisha maana maamuzi yake ya ukaidi ilikuwa yauwe wote kwenye mashua, na injiri aliyo ipiga kule ninawi iliokoa nchi nzima.
Maamuzi yako ni ya Muhimu sana.
Fikiria sana chochote unacho kifanya kina impact either positive or negative.
Maamuzi yako
Neno linasema...
" Usifanye{ Maamuzi ya} haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu." Muhubiri 7:9
Mtu wa Mungu Fanya maamuzi yako kwa utulifu kaa ukijuwa yamebeba hatma ya vizazi vingi.
Nina mwomba Mungu aliyenipa ujumbe huu
Jehovah. Yahweh Jehovah Elohim
Mungu wangu akupe kitu cha kukusaidia.
Amen.
__________
Minister: Enoch Joseph
Life word Ministry
©2017

Mungu wangu akubariki.


Yesu amenipa wakati na nafasi nikutane na wewe Mahali hapa Fb. Bwana amenipa neno hili nije nyumbani kwako...
Yesu anasema...
" Na nyumba yo yote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu; na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu." - Luka 10:5-6
Nami kama Mtumishi Wa Mungu aliye hai. Nakaribia Nyumbani kwako wewe usomaye Profile hii. Natamka Katika Jina la Yesu Amani iwemo katika Nyumba Yako Katika Jina la Yesu.
Amani = Baraka za Mungu, Mafanikio yatokayo Kwa Mungu, Utulivu , Maelewano katika Nyumba yako na Ushirika wa Mungu Roho Mtakatifu uwemo katika Nyumba Yako.
Akiwepo asomaye na kupata Ujumbe Huu anaye stahili Amani hii na Baraka hii ipate na iwemo kwake.
Naiwe kwake katika Jina la Yesu.

Yesu anasema Amani hii nikiiachilia na hayupo mtu anaye istahi itanirejerea lakini itawapata wanao stahili.
Nina omba Katika Jina la Yesu Amani hii iwapate Mamia kwa maelfu ambao Mungu kanipa nafasi kuingia Nyumbani kwao kwa njia hii. Katika Jina la Yesu.
Lakini Yesu anasema...
" waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia." Luka 10:9
Nami natamka Katika Jina la Yesu lipitalo Majina Yeyote ambaye Unaumwa au unamgonjwa nyumbani kwako Pokea Uponyaji Katika Jina la Yesu.
Kuwemo uzima katika Biashara Yako katika Jina la Yesu.
Kuwemo uzima katika Elimu yako katika Jina la Yesu.
Kuwemo uzima katika Uchumi wako Katika Jina la Yesu.
Kuwemo uzima katika Mifugo yako katika Jina la Yesu.
Kuwemo uzima katika kila ukigusacho katika jina la Yesu.
Naiwe kwako katika Jina la Yesu
Amen.
______________________
Minister: Enoch Joseph
Life word Ministry
© 2017

MTEGEMEE MUNGU.



Watu wengi sana huwa wameka tumaini lao kwa wanadamu na wanakwenda mbali kwa kusema una waitaji watu ili uweze kufanikiwa katika maisha yako. Yes according to them is true. Lakini leo nakupa kitu kipya Mtegemee Mungu katika Maisha yako hatakuangusha Yesa maana Yeye ni Mungu Mwaminifu na ni shahidi Mwaminifu.
Neno linasema...
" Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu."~ Yeremia 17:5-6
Usimtegemee Mwanadamu bali mtegemee Bwana.
Usi mfanye mwanadamu kuwa ni kinga yako ya Uchumi bali Bwana ndiyo awe kinga yako Ya uchumi.
Usimfanye Mwanadamu kuwa ni ulinzi wako Bali Bwana awe Mlinzi wako.
Usitegemee msaada wako kuwa utatoka kwa wanadamu au Mwanadamu Bali kwa Mungu.
" Nitayainua macho yangu niitazame milima,
Msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu u katika BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi."
~ Zaburi 121:1-2
Siku zote Hata ukiona kunamilima ambayo inaweza kukusitiri usiitazame wala kuitegemea hiyo milima, hata yajapotokea mafuriko usiitegemee milima hiyo uionayo kwamba itakuhifadhi Mtegemee Bwana.
Haijalishi hiyo milima ni watu wa namna Gani na wapo katika eneo gani katika Maisha yaako. Mtegemee Bwana.
Ndiyo Maana neno linasema...
" Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele." - Zaburi 125:1-2.
Wamtumainio Bwana Ni kama mlima sayuni. Hauta tikisika Bwana atakuzunguka na Kukutunza. Kila unacho hitaji Bwana atakutendea.
My friend Unapaswa kufahamu neno linasema kila kilichopo duniani ikiwepo watu na vyote viujazavyo ni mali ya Bwana.
Neno linasema...
" Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako, Ulimwengu na vyote viujazavyo Ndiwe uliyeupiga msingi wake." Zaburi 89:11
Kila unacho kiona Mungu alikifanya na Msingi wake Mungu aliufanya.
Hivyo ukimtegemea Mungu Mungu atatumia chochote au Yeyote aliye Muumba kukufikishia hitaji la Maisha Yako.
Ndiyo maana neno linasema...
" Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, Mara moja tena, ni kitambo kidogo tu, nami nitazitikisa hizo mbingu, na hii nchi, na bahari, na nchi kavu; nami nitatikisa mataifa yote, na vitu vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja; nami nitaijaza nyumba hii utukufu, asema Bwana wa majeshi. Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi." Hagai 2:6-8
Mungu kitu atafanya atakileta chochote unacho kiitaji kitakuja. Kitakuja kwa njia gani? Ninacho juwa Mungu atafanya njia. Sijuwi ni nani atakaye leta huo msaada au ujumbe unao uhitaji. Bali ninacho juwa Atamtuma Mjumbe Kwako.
Bwana atakutendea.
Mtegemee Bwana.
Na Bwana atakupa aja ya Moyo wako.
Akikutendea Bwana kupitia angle yeyote Heshima na Utukufu mrudishie Bwana.
Ninachojuwa ukimtegemea Bwana na Bwana atakapigania wewe nawe utamtukuza Bwana kwa Ukuu wake.
Amen.
Barikiwa na Yesu.
_________________
Minister: Enoch Joseph
Life word Ministry
©2017.

Mwamini MUNGU,Sema NENO na Usiwe na Shaka moyoni bali amini usemalo nalo litakuwa.




Unaweza ukawa unapitia katika kipindi fulani katika Maisha yako na ukawa hauna namna ya kufanya au umeshindwa kujuwa nini cha kufanya. Neno la Bwana limekujia leo kuwa una vitu vitatu vya kuwa navyo na vitakavyo tenda chochote utakacho.
i} Mwamini Mungu/ Kumwamini Mungu. Trust God.
ii} Sema Neno/ Azina ya Nguvu iliyopo katika Kusema.
iii} Kuwa na imani{ usiwe na shaka bali uwe na hakika}
Ukiwa na haya matatu hakuna mahali utakapo pita au kupitia ukashindwa kuvuka.
Neno linasema...
" Yesu akajibu, ...Mwaminini Mungu. Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia{ atakaye sema} mlima huu{ Tatizo hili au lile} , Ng'oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake." Marko 11:22-23.
Mwamini Mungu alicho sema ni amina na kweli. Ipo nguvu kubwa katika kusema.
Alicho sema Yesu anauhakika na alicho kisema na ikiwa unaweza kuamini wasemacho watu si zaidi kuamini asemacho Yesu?
Semesha huo mlima unao uona mbele yako ungoke nao utakutii. Semesha miti{falme} zote zinazo kusumbuwa ziwe tambalale nazo zitakutii.
Nakuombea Umwami Mungu Katika Jina la Yesu.
Nakuombea uwe hodari katika Bwana katika Jina la Yesu.
Ufanikiwe katika Jina la Yesu.
Ubarikiwe
___________________
Minister: Enoch Joseph
Life word Ministry
©2017.

Ipo siri na Nguvu kubwa sana kwenye Kuamini na Kushukuru Mungu.

Image may contain: one or more people and text
Ipo siri na Nguvu kubwa sana kwenye mambo mawili.
i} Kuamini
ii} Kushukuru Mungu.
Yohana 11:40-42.
_______________________
Yesu Mara nyingi amekuwa akisisitiza kwa habari ya Kuamini maana ina nafasi kubwa sana kwa Maombi ya mtu kujibiwa.
Nataka uone hili jambo kwa kuangalia Muujiza Mkubwa wa kufufua alioufanya Yesu.
Yesu akamjibu { Martha} “Sikukuambia kama ungeamini ungeuona utukufu wa Mungu?”
¶- ona kitu hapa kumbe kuamini kuna sababisha utukufu wa Mungu kuonekana katika Jambo ambalo unamuomba Mungu. Na ukitaka kuuona utukufu wa Mungu. Mfano Uponyaji,kufufuliwa kwa vilivyo kufa maishani mwako, na kufanikiwa katika jambo maishani mwako. Na kujibiwa maombi yako.
Kwa lugha nyingine ni kwamba kama hauta amini ni ngumu kuuona utukufu wa Mungu. Ndiyo maana Yesu alipo ona imani imeyumba na aipo kwa martha akaamua kumpatia neno linalo weza kumrudishia imani yake.
Ivyo katika Maombi yake alishughulikia Mambo mawili. Imani na Kumshukuru Mungu.
Yesu akaangalia mbinguni akasema, “Baba ninakushukuru kwa kunisikia. Ninajua ya kuwa huwa unanisikia wakati wote, lakini nimesema hivi kwa faida ya hawa walio hapa, ili wapate kuamini ya kuwa umenituma.”
Yesu alikuwa anaomba marakwa mara Baba alikuwa anamsikia. Tambua maombi unayo yaomba siku zote Mungu huwa anasikia na ni akiba yako.
Lakini alitaka watu wajuwe na kuamini kuwa leo siyo mala ya Kwanza kuzungumza na Baba yake. Na watu wakijuwa ya kwamba huwa siku zote huwa ana zungumza na Baba yake kiwango chao cha imani kitaongezeka na kutengeneza njia kwa Muujiza kutokea.
Unaweza usijuwe kuwa imani ni Muhimu kwa anaye ombewa, anaye shuhudia na Muombaji. Mpaka utakapo jiuliza Kwanini Yesu katika Maombi yake alisema Baba ninakushukuru kwakunisikia. Akionesha Yeye imani yake ipo sawa anajuwa Mungu amemsikia. Lakini akasema ninajuwa yakuwa siku zote huwa unanisikia. Ameyasema hayo ili alio nao waamini yakuwa Mungu ndiye aliye Mtuma.
Kwahiyo kuna mambo mawili hapa kwenye kuamini.
i~ Kuamini Mungu anaweza kutenda Muujiza katika Maisha ya Muombaji na anaye ombewa .
ii~ Kumwamini Mtumishi anaye omba yakuwa anatenda atendayo kwa Msaada wa Mungu na ametumwa na Mungu. Unaweza ukafikili kibali au utambulisho hauna Maana Mungu ilibidi amtambulishe Yesu alipokuwa akibatizwa ili wamwamini na kumpokea.
Imani ni Muhimu sana ndio maana mahali pengine alipo gundua watu wa mahali imani yao ni hasi/-ve aliomba waondolewe maana kutokuwa na imani ni kikwazo.
Lakini Mungu anapendezwa sana na shukrani mshukuru Mungu na kadri utakapo kuwa unamshukuru Mungu ndivyo utakavyo kuwa unapalilia Muujiza wako.
Ivyo ukitaka Muujiza utendeke katika maisha yako na kuuona utukufu wa Bwana katika kila eneo.
¶- hakikisha imani imekaa sawasawa ikiwezekana vipige vita vya imani na ushinde.
¶- Ukiona unapata shida au unaoomba nao wape neno la ushuhuda jinsi Mungu alivyo kusikia nyuma na Mambo aliyo tenda pamoja nawe nyuma.
¶- Mshukuru Mungu. Yes Tumia mda wa kutosha mshukuru Mungu.
Amen.
Namuomba Mungu akupe kitu cha kukusaidi katika ujumbe huu katika jina la Yesu.
Amen.
___________________
Minister: Enoch Joseph
Life word Ministry.
©2017

Ninyi wenye kumkumbusha Bwana Msiwe na Kimya

Ninyi wenye kumkumbusha Bwana Juu ya Mambo yahusuyo, Maisha yenu, Familia zenu, Koo zenu, na Jamii zenu Msiwe na Kimya mpaka atakapo fanya imara Maisha yako, Familia yako, Ukoo wako, na Jamii Yako.
_________________________________
Nimekuwa nikisikia wapendwa wakifundishwa jifunze kunyamaza na wengi huwa wanapoke neno hili kwa namna ya kufarijiwa kuwa ili wapone yale wanayo pitia.
Ni kweli kabisa unapaswa kujifunza kunyamaza kwasababu hata neno linasema...
" Hata mpumbavu akinyamaza huonekana ana hekima;akifunga mdomo wake huonekana kuwa mwenye akili."- Mithali 17:28.
Yes hii ni faida moja wapo ya kunyamaza hatakama ulikuwa ni mpumbavu na hauna akili kunyamaza kunakupa credit ya kuwa Mwenye hekima na mwenye akiri. Watu watakuheshimu pia kwa maamuzi haya mazuri japo yanayo umiza usipjuwa upande wa pili nini ufanye unapokuwa umekwisha nyamaza.
Lakini pia Neno la Mungu linasema...
" Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya." ~ Kutoka 14:13-14.
Hapa wana wa Israel waliambiwa Mambo kadhaa
- Msiogope- Aupaswi kuogopa Mtu wa Mungu.
-Simameni tu. - Mtu aliye simama ni mkakamavu, Yupo tayari kutembea na kusonga mbele, na ni hodari.
Lakini waliambiwa wajiandae kuona Wokovu wa Bwana pale atakapo waangamiza maadui zao.
Kitu nataka uone ni kwamba walinyamaza Yes hawakubishana wala kusemezana na maadui Bali Mungu alishughulika na maadui zao.
Upande ulio jificha ambao unapaswa kuufahamu ni kwamba. Hakikisha unasimama na Bwana, Hakikisha unakuwa Hodari katika Bwana, na kila wakati usinyamaze kumsemesha Bwana ili Bwana akutendee.
Mtu wa Mungu neno linasema...
" ...ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya; wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani. Bwana ameapa kwa mkono wake wa kuume, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi..."
~Isaya 62:6-8
Nataka uone Bwana ameapa kuwashughulikia maadui zako lakini hili ni muhimu sana usinyamaze kimya endelea Kumbusha Bwana mpaka utakapo ona Bwana amekutendea na kukufanya imara.
Mpaka utakapona Bwana amewashughulikia Maadui zako.
Usinyamaze kimya endelea kumkumbusha Bwana.
Amen.
Bwana Mungu wa Israel akupiganie na kukutendea wewe Katika Jina la Yesu.
Barikiwa.
_____________________
Minister: Enoch Joseph
Life word Ministry
©2017.

Urithi wa watumishi wa Mungu

URITHI WA WATUMISHI WA MUNGU. ------------------------------------------------------------ Hii wengi hawafahamu lakini leo fahamu japo k...