Unafanyaje Mungu akikutendea kitu. Unapaswa kumshukuru Mungu.
Neno linasema...
" Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao."
~ Mathayo 8: 4.
Yesu alipo mponya Mtu Mwenye ukoma akampa maelekezo ya msingi ambayo anapaswa afanye.
#A- Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani.
- Mathayo 9:28-31. aliwaponya wenye upofu kisha aka waambia mtu yeyote asijuwe lakini wao wakaeneza habari zile kila mtu akajuwa. Kwahiyo alipo sema usimwambie mtu ilikuwa ni jambo moja but condition ya msingi ilikuwa nenda ukajioneshe kwa Kuhani.
Swali Yesu akikuponya unaenda kujionesha kwa nani? Pengine unaweza sema Yesu amekuponya kupitia huyo kuhani. Bado swali ni Je umeenda kujionesha kwake na kumshuhudia Bwana Yesu aliyo tenda kupitia Yeye.
★ Kumbuka kwa kuhani Kuna ulinzi unapoenda kwa kuani kujionesha unaripoti kwa mlinzi achukuwe zamu ya ulinzi.
Ndiyo maana neno linasema...
" Nimeweka walinzi( Kuhani) juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya;"
~Isaya 62: 6.
NB. Kumbuka kuhani wa Bwana anaweza kuwana cheo cha.
i- Mtume
ii-Nabii
iii-Mwinjiristi.
iv- Mchungaji
v- Mwalimu.
Yesu akamwambia akajioneshe kwa Kuhani.
#B. Ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.
Kumbe unapo enda kujionesha kwa Kuhani unapaswa kuwa na sadaka kama alivyoamuru Musa. Kumbuka haya ni Maneno ya Yesu.
Sadaka utakayo itoa itakuwa ushuhuda kwao. Ushuhuda wako utaambatana na sadaka. Kwa lugha nyepesi sadaka yako itakuwa ushuhuda kwa Kuhani. sadaka hubeba ushuhuda.
Kumbuka Mungu akikutendea jambu Neno shukrani kwa Mungu lisikosekane kwako.
Linda Muujiza wako kwa kumshukuru Mungu
Tengeneza Muujiza mwingine kwa kumshukuru Mungu.
Amen.
Ubarikiwe na Yesu.
_________________________
Minister: Enoch Joseph
Life word Teaching Ministry
★2017.
"It is the Spirit who gives life; the flesh profits nothing. The words that I speak to you are spirit, and they are life." ~John 6:63
Wednesday, 13 December 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Urithi wa watumishi wa Mungu
URITHI WA WATUMISHI WA MUNGU. ------------------------------------------------------------ Hii wengi hawafahamu lakini leo fahamu japo k...

-
Bwana Yesu asifiwe sana! Leo nataka tujifunze juu ya “Mwongozo wa kutafakari na kuombea ndoto zenye UZINIFU AU UASHERATI ndani yake”....
-
SEMINA YA NENO LA MUNGU UWANJA WA TANGANYIKA PACKERS - DAR ES SALAAM MWL.CHRISTOPHER MWAKASEGE TAREHE 15 OKTOBA 2017 *SIKU YA NA...
-
Ninyi wenye kumkumbusha Bwana Juu ya Mambo yahusuyo, Maisha yenu, Familia zenu, Koo zenu, na Jamii zenu Msiwe na Kimya mpaka atakapo f...
No comments:
Post a Comment