Bwana Yesu asifiwe sana!
Leo nataka tujifunze juu ya “Mwongozo wa kutafakari na kuombea ndoto zenye UZINIFU AU UASHERATI ndani yake”.
Maneno haya ‘uzinifu na uasherati’ yanahusu ufanyikaji wa tendo la ndoa usio halali kibiblia. Uzinifu linatumika zaidi wakati tendo la ndoa limefanywa na mtu ambaye hajaoa au hajaolewa. ‘Uasherati’ linatumika zaidi wakati tendo la ndoa limefanywa nje ya ndoa na mtu ambaye ameoa au ameolewa.
Mtu anayepata ndoto zenye mambo hayo, huwa zina madhara makubwa sana ya kiroho, na ya kimwili – kwa aliyeota ndoto hizo!
Kumbuka kwamba: Neno la Mungu la biblia, kwa kushirikiana na Roho Mtakatifu, linatuongoza kujua namna ya kutafsiri na kuziombea ndoto za aina yo yote – ambazo ni pamoja na hizi zenye mambo ya uzinifu au uasherati ndani yake.
Ni muhimu kwako kupata nafasi ya kusoma, na kutafakari mistari ya biblia, ambayo nimeambatanisha na somo la leo. Hebu tujifunze somo la leo kwa mtiririko ufuatao:
(1) Ukiota unazini kwenye ndoto maana yake nini? Ina maana ya kwamba
(a) Umeunganishwa kiagano na roho ya (au pepo la) uzinifu au uasherati – kufuatana na aina ya mtu uliyekuwa unazini naye.
Neno linasema…
“Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.”
~1 Wakorintho 6:16,17.
(b) Unapoteza uwezo wa kufaidi matunda ya ufalme wa mbinguni.
Neno linasema…
“ Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, 10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.”
~ 1 Wakorintho 6:9
(c) Ni ishara ya kwamba mwili wako umepandikizwa mbegu ya kukuzuia usiweze kuomba, au usiwe mwombaji.
Neno linasema…
“ 18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.”
~ 1 Wakorintho 6:18 – 20.
(d) Umepandikizwa roho na mbegu ya kumwasi Mungu tunayemwabudu katika Yesu Kristo.
Neno linasema…
“10 Hivyo Edomu wakaasi chini ya mkono wa Yuda, hata leo; wakaasi na Libna zamani zizo hizo chini ya mkono wake: kwa sababu alikuwa amemwacha Bwana, Mungu wa baba zake. 11 Tena ndiye aliyefanya mahali pa juu milimani pa Yuda, na kuwaendesha katika uasherati wenyeji wa Yerusalemu, na kuwakosesha Yuda.”
~ 2 Mambo ya Nyakati 21:11
Na Pia neno linasema…
“Tena umezini na Wamisri, jirani zako, wakuu wa mwili; ukaongeza mambo yako ya kikahaba, ili kunikasirisha.
~ Ezekiel 16:26
(e) Ni njia ya kupanda ‘mbegu’ ya uzinzi, au ya uasherati, ambayo isipoondolewa kwa damu ya Yesu, itachipuka katika maisha ya baadaye ya mtu aliyeota hiyo ndoto.
Neno linasema…
“18 Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi. 19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;”
~Mathayo 15:18, 19
Pia katika Mathayo 5:27, 28
Neno linasema...
“27 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; 28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”
~ Mathayo 5:27, 28
(2) Ukiota unazini kwenye ndoto na ndugu yako wa karibu – kama baba au mama mzazi, au dada yako, au kaka yako, au mkwe, au mjomba au mke wa mjomba….ina maana ya kwamba:
(a) Unaandamwa na roho ya kukataliwa na kutengwa na wale wa imani moja na wewe kiroho!
Neno linasema…
“1 Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye. 2 Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo. 3 Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo. 4 Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu; 5 kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu.”
~ 1 Wakorintho 5:1 – 5.
(b) Utasumbuliwa na magonjwa au hatari zingine kwenye mwili wako kwa lengo la kukuua. Soma 1 Wakorintho 5:1 – 5.
(c) Unaandamwa na roho ya mauti.
Neno linasema…
“11 Na mtu mume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao. 12 Na mtu mume akilala na mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauawa; wamefanya yaliyo uchafuko; damu yao itakuwa juu yao. 13 Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao. 14 Tena mtu mume akimwoa mke pamoja na mama yake, ni uovu mkuu; watachomwa moto, yeye mume na hao wanawake pia; ili kwamba usiwe uovu kati yenu.”
~ Walawi 20:11 – 14.
(d) Unaandamwa na roho ya kurithi iliyobeba uovu.
Neno linasema…
“17 Tena mtu mume akimwoa umbu lake, binti ya baba yake, au binti ya mama yake, na kuuona utupu wake, na huyo mwanamke kauona utupu wake huyo mume; ni jambo la aibu; watakatiliwa mbali mbele ya macho ya wana wa watu wao; amefunua utupu wa umbu lake; naye atauchukua uovu wake… 19 Usifunue utupu wa umbu la mama yako, wala umbu la baba yako; kwa kuwa huyo amefunua utupu wa jamaa yake ya karibu; watauchukua uovu wao. 20 Tena mtu mume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake; watauchukua uovu wao; watakufa bila kuzaa mwana.”
~Mambo ya Walawi 20:17, 19, 20.
(e) Utasumbuliwa na tatizo la kutokuzaa watoto.
“20 Tena mtu mume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake; watauchukua uovu wao; watakufa bila kuzaa mwana. 21 Tena mtu mume akimtwaa mke wa nduguye, ni uchafu; ameufunua utupu wa nduguye; hao watakuwa hawana wana.”
~Mambo ya Walawi 20: 20, 21.
(f) Unafungulia roho ya ukahaba.
Neno linasema…
“Usimnajisi binti yako, ili kumfanya awe kahaba; isiwe hiyo nchi kuuandama ukahaba, na nchi kujawa na uovu mkuu.”
~Mambo ya Walawi 19:29
(g) Umepandikizwa au unapandikizwa roho au pepo la kukataliwa na waliookoka (Ikiwa uliyeota ndoto hiyo umeokoka); au wakristo wanaokufahamu.
Neno linasema…
“9 Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi. 10 Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. 11 Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye. 12 Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani? 13 Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu. Ninyi mwondoeni yule mbaya miongoni mwenu.”
~1 Wakorintho 5:9 – 13
(3) Ukiota ndoto unazini au unafanya uasherati na mtu wa “imani” nyingine maana yake nini? Ndoto ya namna hii ina maana ya kuwa kuna roho au pepo lililoingia nafsini mwako ili.
(a) Kuua na kuharibu imani yako ili uiache na ufuate imani nyingine ya huyo uliyezini naye kwenye ndoto.
Neno Linasema…
“15 Usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi, watu wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, na kuitolea sadaka miungu yao; mtu mmoja akakuita, ukaila sadaka yake. 16 Ukawaoza wana wako binti zao, nao binti zao wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, wakawavuta wana wenu wafanye uzinzi na miungu yao.”
~Kutoka 34:15, 16
Pia Neno linasema…
“1 Bwana, Mungu wako, atakapokutia katika nchi uendayo kuimiliki, atakapoyang'oa mataifa mengi watoke mbele yako, Mhiti, na Mgirgashi, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, mataifa saba makubwa yenye nguvu kukupita wewe; 2 wakati Bwana, Mungu wako, atakapowatoa mbele yako, nawe utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao; 3 binti yako usimpe mwanawe mume, wala usimtwalie mwanao mume binti yake. 4 Kwa kuwa atamkengeusha mwanao mume asinifuate, ili wapate kuabudu miungu mingine; ndipo itakapowaka hasira ya Bwana juu yenu, naye atakuangamiza upesi.”
~Kumbukumbu ya Torati 7:1 – 4
Pia Neno linasema…
“1 Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu; 2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao.”
~ Hesabu 25:1,2
Pia Neno linasema…
“1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, 2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda. 3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo. 4 Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake. 5 Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni… 7 Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni. 8 Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu. 9 Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili,”
~1 Wafalme 11:1 – 5, 7 – 9.
(b) Kukufanya urudi nyuma kiroho, na usiweze kumfuata vizuri Mungu unayemwabudu katika Kristo Yesu.
“1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, 2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda… 6 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.”
~1Wafalme 11:1, 2, 6.
(c) Inafungua mlango wa maadui kuinuka juu yako na dhidi yako, na kupata nafasi ya kukusumbua na kukufanya ukose utulivu.
“1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, 2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda…14 Ndipo Bwana akamwondokeshea Sulemani adui, Hadadi Mwedomi; yeye alikuwa wa wazao wake mfalme wa Edomu…23 Tena, Mungu akamwondokeshea adui mwingine, Rezoni mwana wa Eliada, aliyemkimbia bwana wake Hadadezeri mfalme wa Soba.”
~1 Wafalme 11:1, 2, 14, 23.
(d) Inafungulia pepo la mauti likiwa na lengo la kukua, kwa nia ya kujitafutia sifa kwa ‘mungu’ wake.
Neno linasema…
“1 Basi Israeli akakaa Shitimu, kisha watu wakaanza kuzini pamoja na wanawake wa Moabu; 2 kwa kuwa waliwaalika hao watu waende sadakani, sadaka walizowachinjia miungu yao; watu wakala chakula, wakaisujudu hiyo miungu yao. 3 Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli. 4 Kisha Bwana akamwambia Musa, Watwae wakuu wote wa hao watu, ukamtungikie Bwana watu hao mbele ya jua, ili kwamba hizo hasira kali za Bwana ziwaondokee Israeli. 5 Basi Musa akawaambia waamuzi wa Israeli, Waueni kila mtu watu wake waliojiungamanisha na Baal-peori. 6 Na tazama, mtu mmoja miongoni mwa wana wa Israeli akaja na kuwaletea nduguze mwanamke Mmidiani mbele ya macho ya Musa, na mbele ya macho ya mkutano wote wa wana wa Israeli, hapo walipokuwa walia mbele ya mlango wa hema ya kukutania. 7 Naye Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, alipoona jambo hilo, akaondoka hapo katikati ya mkutano, akashika fumo mkononi mwake; 8 akamwandama huyo mtu wa Israeli na kuingia ndani ya hema nyuma yake, naye akawachoma wote wawili kwa fumo lake, yule mume wa Israeli na huyo mwanamke kati ya tumbo lake. Basi pigo likazuiwa kwao wana wa Israeli. 9 Nao waliokufa kwa hilo pigo walikuwa watu elfu ishirini na nne hesabu yao. 10 Kisha Bwana akanena na Musa, akamwambia, 11 Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, amezigeuza hasira zangu zisiwe juu ya wana Wa Israeli, kwa kuwa alikuwa na wivu kati yao kwa wivu wangu mimi, hata nisiwaangamize wana wa Israeli katika wivu wangu. 12 Basi kwa hiyo, sema, Tazama, nampa yeye agano langu la amani; 13 tena kwake yeye, na kizazi chake baada yake, litakuwa agano la ukuhani wa milele; kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya Mungu wake, na kuwafanyia upatanisho wana wa Israeli.”
~Hesabu 25:1 – 13.
(e) Inafungulia roho ya wivu
(Kutoka 34:14 – 16 na Hesabu 25:1, 2, 10, 13)
Na roho hiyo inayozaa ugomvi wenye kisasi mara kwa mara
“Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.”
~Yakobo 3:16
(4) Ukiota ndoto unazini na mnyama – ina maana gani? Kwa mfano – kuna mama mmoja aliniandikia kuwa aliota yuko uchi kwenye banda la ng’ombe, na ng’ombe dume akazini naye! Alipoamka toka usingizini alisikitika sana!
Ukiota ndoto za kuzini na mnyama maana yake ni hii:
(a) Umevamiwa na unaandamwa na roho ya mauti,
Neno linasema…
“19 Mtu awaye yote alalaye na mnyama sharti atauawa.”
~Kutoka 22:19
Pia Neno linasema…
“15 Tena mtu mume akilala na mnyama, hakika atauawa; nanyi mtamwua huyo mnyama. 16 Tena mwanamke akimkaribia mnyama ye yote, na kulala pamoja naye, mtamwua huyo mwanamke, na mnyama pia; hakika watauawa; damu yao itakuwa ni juu yao.”
~Mambo ya Walawi 20:15,16.
(b) Umechafuliwa kiroho ili uwepo wa Mungu ukae mbali na wewe.
Neno linasema…
“23 Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko”
~Mambo ya Walawi 18:23
(c) Unapandikizwa laana.
“21 Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina.”
~Kumbukumbu ya Torati 27:21.
(5) Madhara ya ziada yanayoweza kumpata MWANAUME akiota ndoto anazini au anafanya uasherati ni pamoja na:
(a) Kupata tatizo la kutoweza kutumia akili vizuri (Mithali 6:32, 33), katika kufikiri kimaisha!
Neno linasema…
“32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake. 33 Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; Wala fedheha yake haitafutika.”
~ Mithali 6:32, 33
(b) Maendeleo yake kiroho na kimaisha na kifikra yanakwama kwa kuwa nafsi yake ‘inanaswa’
Neno linasema…
“26 Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu anase nafsi yake iliyo ya thamani”
~Mithali 6:26.
Nafsi yake iliponasia ndipo panapoweka kipimo cha maendeleo yake
Neno linasema…
“ Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.”
~3 Yohana 1:2.
(c) Nguvu za kiume za uzazi zinapungua au zinapotea kabisa
“3 Maana midomo ya malaya hudondoza asali, Na kinywa chake ni laini kuliko mafuta; 4 Lakini mwisho wake ni mchungu kuliko pakanga; Ni mkali kama upanga wa makali kuwili. 5 Miguu yake inatelemkia mauti; Hatua zake zinashikamana na kuzimu; 6 Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutanga-tanga wala hana habari. 7 Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Wala msiache maneno ya kinywa changu. 8 Itenge njia yako mbali naye, Wala usiukaribie mlango wa nyumba yake. 9 Usije ukawapa wengine heshima yako, Na wakorofi miaka yako; 10 Wageni wasije wakashiba nguvu zako; Kazi zako zikawa ndani ya nyumba ya mgeni;”
~Mithali 5:3 – 10
(6) Madhara ya ziada yanayoweza kumpata MWANAMKE, ikiwa ataota anazini, au anafanya uasherati kwenye ndoto, ni pamoja na pepo kupata nafasi ya kuingia, na kukaa kwenye kizazi chake
“20 Tena mtu mume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake; watauchukua uovu wao; watakufa bila kuzaa mwana. 21 Tena mtu mume akimtwaa mke wa nduguye, ni uchafu; ameufunua utupu wa nduguye; hao watakuwa hawana wana.”
~Mambo ya Walawi 20: 20, 21
Na pia kumletea madhara kama ifuatavyo:
(a) Kuvuruga mzunguko wake wa damu ya mwezi;
(b) Kuweza kuharibu mimba –ikiwa – huyo mwanamke aliyeota ndoto alikuwa mja mzito alipokuwa akiota ndoto hiyo;
(c) Kuvuruga uwezekano wa kupata mimba – ikiwa ameolewa;
(d) Kuharibu viwango vya utendaji kazi wake kama mwanamke akiwa nyumbani kwake;
(e) Kupandikizwa magonjwa kwenye kizazi chake, au/na kwenye damu yake
(7) Ukiota unazini au unafanya uasherati kwenye ndoto wakati umekwisha chumbiwa au umekwisha chumbia; au wakati zimebaki siku chache za kufanyika kwa harusi yako – ujue maana ya ndoto hiyo ni hii:
KWAMBA: Kuna pepo lililopata nafasi kwako, ili kuvuruga mipango yako ya harusi isifanyike; au hata kama utaolewa, au utaoa – hilo pepo litatengeneza mazingira ya wewe kuachika, au kuachana na huyo mwenzi wako!
“16 Mtu akimshawishi mwanamwali, aliyeposwa na mume, na kulala naye, lazima atatoa mahari kwa ajili yake ili awe mkewe.”
~Kutoka 22:16
(8) Ukiota ndoto unazini, au unafanya uasherati na kichaa au mchawi – ujue maana ya ndoto hii ni; KWAMBA: Shetani anapandikiza hila zake kwenye maisha yako, ili kukusababishia ukataliwe na watu wako!
“ 6 Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake.”
~ Mambo ya Walawi 20:6
(9) Ikiwa ‘eneo’ ulilofanyia uzinifu au uasherati kwenye ndoto uliyoota linaeleweka …yaani kama nyumbani, ofisini, jikoni, makaburini, darasani – nakadhalika – ndoto hiyo inakupa ujumbe gani wa ziada?Ndoto kama hii – yenye kukuonyesha uzinifu, au uasherati ulipofanyika, inataka ujue ya kuwa – kiroho eneo hilo ‘limenajisika’, na ‘kuchafuka’, na lisiposafishwa kwa damu ya Yesu mapema, litatoa nafasi kwa mapepo kujitengenezea ‘kituo’ chao!
“ 20 Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye. 21 Nawe usitoe kizazi chako cho chote na kuwapisha kwa Moleki, wala usilinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi Bwana. 22 Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. 23 Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko. 24 Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote; 25 na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa. 26 Kwa hiyo mtazishika amri zangu na hukumu zangu, wala msifanye machukizo hayo mojawapo; yeye aliye mzalia, wala mgeni aketiye kati yenu; 27 (kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;) 28 ili kwamba hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu. 29 Kwani mtu awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao. 30 Kwa ajili ya hayo yashikeni mausia yangu, ili kwamba msifanye kabisa desturi hizi zichukizazo mojawapo, zilizotangulia kufanywa mbele zenu, wala msijitie unajisi katika mambo hayo; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”
~Mambo ya Walawi 18:20 – 30
Na pia Neno linasema…
“2 kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake.”
~Ufunuo wa Yohana 19:2
(10) Hatua zifuatazo zitakusaidia katika kupanga mambo ya kuomba juu ya ndoto za namna hii:
(a) Fanya maombi ya Toba kwa ajili ya mlango uliofunguka na ukaota ndoto za namna hii
(b) Vunja kwa damu ya Yesu aina yo yote ya muunganiko wa kiagano, kati ya nafsi yako (uliyeota ndoto) na roho ya kipepo iliyojiunganisha na nafsi yako, kwa kupitia kwenye ndoto hiyo
(c) Kemea kwa jina la Yesu kila aina ya roho ya kipepo iliyokuja kwako kwa kupitia hiyo ndoto;
(d) Haribu kwa damu ya Yesu aina yoyote ya mbegu ya uzinifu, au ya uasherati au ya ukahaba iliyopandikizwa ndani yako kwa njia ya ndoto hiyo
(e) Omba uponyaji wa eneo lo lote lililopata madhara kwenye roho yako, au kwenye nafsi yako, au kwenye mwili wako, au kwenye mahusiano yako na watu wengine, au kwenye mipango yako, nakadhalika
(f) Omba neema ya Mungu ikusaidie kurejesha kwa upya mahusiano yako na Mungu katika Yesu Kristo
(g) Omba utakaso wa damu ya Yesu ufanyike kwenye eneo ambalo kufuatana na ndoto hiyo – uzinifu ulifanyika hapo.
LA KUKUMBUKA: Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kukupanulia wigo wa ufahamu, juu ya eneo lingine linalohusu ndoto za namna hii ambalo sijaligusia hapa. Mungu azidi akubariki.
Amen
Imetolewa toka Fb Page ya Mwalimu Christopher Mwakasege
Na kuongeza maandishi kama yalivyo andikwa kwenye Biblia Mahali aliposema Kasome Nimekuwekea hapa Usome.( reference from The Bible) Pia usiache kwenda kwenye Biblia Yako Kusoma.
Utukufu na Heshima Vina Wewe Mungu Kwa kupitisha Chakula Hiki Kwa Mwl. Christopher Mwakasege. Cha wakati na chenye msaada Mkubwa na Chenye Nguvu ya Ukombozi Ndani yake. Na Kunifikia Mimi Minister : Enoch Joseph na hata kuwafikia wengine wote Wasomao.
Thank You Jesus.
Thank You Dad Mwalimu C.Mwakasege.