Thursday, 7 September 2017

Mtumikie Bwana Mda wote

Shalom
Ni asubuhi njema...
Neno linasema...
" Bwana, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia." ~ Zaburi 5:3
Daudi Mtumishi wa Mungu na Mfalme ilikuwa kilasiku asubuhi anasogea Mbele za Bwana na Kuomba. Kupeleka Mahitaji yake kwa Bwana.
Nimuhimu kila iitwapo asubuhi kabla ya kufanya jambo lolote kujisogeza kwa Bwana na Kuomba na kumkumbusha Bwana Mahitaji Yako.
Uwe na Uhakika Mungu hatanyamaza kimya atakusikia Kuomba Kwako. Na kwakumpa mda wako wa kwanza wa siku kwa kuomba unakuwa umetoa mda wako sadaka kwa Bwana.
Daudi aliishi maisha haya....
Neno linasema....
" ...‘I have found David son of Jesse a man after my own heart; he will do everything I want him to do. "
" ...akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote."~ Matendo 13:22.
Moyo wa daudi ulimpenda Mungu. Unaye mpenda unampa nafasi ya Kwanza.
Ninakuombea katika Jina la Yesu.
Moyo wako Upende Mungu Katika Jina la Yesu.
Mwambie Mungu ahsante kwa Ulinzi wako.
Mkumbushe Bwana Mahitaji yako anapo wahudumia wengine asikusahau na wewe.
Omba omba
Kwakuwa Bwana amekupa nafasi kusoma huu ujumbe Ujue lipo neno kwaajiri yako.
Mungu akuhudumie Katika Jina la Yesu.
Ubarikiwe na Yesu.
_________________________________
Minister: Enoch Joseph
Life word Ministry
©2017.

No comments:

Post a Comment

Urithi wa watumishi wa Mungu

URITHI WA WATUMISHI WA MUNGU. ------------------------------------------------------------ Hii wengi hawafahamu lakini leo fahamu japo k...