Friday, 8 September 2017

Tazama jambo Jipya Duniani

Nimeona jambo katika Dunia hii na kizazi hiki. Watu wanatamani Mungu atambuliwe kwa Majina yao. Siyo Mbaya ikiwa kweli wanaye Mtumikia ndiye Jehovah - The LORD mighty in battle
___________________
Ninamshukuru Mungu kwa kunionesha Jambo hili ni Muhimu sana watu wa Kizazi hiki wafahamu Kuna hali ya Hewa imechafuliwa sana katika ulimwengu wa roho.
Kuna waganga wa kienyeji ambao sasa wanavaa suti na wapo kwenye majengo yanayo itwa makanisa. Wamesababisha watu wengi sana hasa wasio na Macho kuangamia.
Kitu naTaka ujuwe kuna Umuhimu wa Kum
juwa Mungu kwa kiwango cha kuwa na personal Relation na Mungu. Yani ujuwe ni Mungu Yupi unaye Mtumikia. Ndiyo maana Musa alipo kuwa amepewa wajibu wa kwenda kuwatoa wana wa israel na kuwapeleka katika nchi ya kanani.
Alimuuliza Bwana wakiniuliza ni Mungu yupi aliye kutuma. Bwana akamwambia Yeye ni Yahweh: “I AM WHO I AM.
Chamsingi nataka Ujiulize Ukisikia Mtu au Mtumishi ana muadress Mungu kwa Jina lake Huwa Huwa unajiuliza maswali ya Msingi au kwako ukiona Muujiza umefanyika kupitia Mtumishi huyo unaamini tu kuwa huyo ndiye Mungu wa kweli
Inawezekani kweli atendaye Muujiza kwa Kupitia Mtumishi huyo ni Mungu ~ Elohim - Mungu aliye ziumba Mbingu na nchi.
Swali la msingi ni Mtume paulo aliuliza.
" Je, ninyi ni wajinga kiasi hiki? Baada ya kuanza na Roho wa Mungu, sasa mnataka kuwa wakamilifu kwa uwezo wenu wenyewe?" Wagaratia 3:3
Yaani Yote kizazi hiki kilichofundishwa wazi wazi Juu ya Mungu. Sawa sawa na Maandiko kinaona hayafai. Bali kinataka Kumuona Mtu fulani wanaye Muona na wakamtumikia Mungu wake.{ Mungu wa Peter, Mungu wa John etc.} Amini ni kwambiayo Hawataki kusikia Tena habari ya Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Eliya, etc. }
Kizazi hiki kinapaswa kufahamu Mungu ni Mungu ashikaye Maagano. Yapo maagano alifanya na Ibrahimu, Yapo maagano alifanya na Yakobo||Israel etc.
Sasa ona namna hii ikiwa mtumishi Huyo alianza na Mungu kisha akamaliza na kufanya agano na kuzimu. Unajuwa unapo kiri Mungu wa huyo mtumishi ndiyo Mungu wako. Ikiwa amefanya agano na kuzimu kwa siri unaungwa pamoja na kuzimu kwa Maneno ya kinywa chako. Kila unapo kiri na kinywa chako.
Chunga sana.
Shetani naye yupo kazini.
Kuwa makini sana.
{ 1 Yohana 4:1.}
Asikiaye na Afahamu
Maneno Roho akiambia Kizazi Hiki.
_____________________________________
Minister : Enoch Joseph
Life word Ministry
©2017.

No comments:

Post a Comment

Urithi wa watumishi wa Mungu

URITHI WA WATUMISHI WA MUNGU. ------------------------------------------------------------ Hii wengi hawafahamu lakini leo fahamu japo k...