Thursday, 7 September 2017

Mungu aweza kukufanikisha katika Kila eneo la maisha yako kwa kukupa akili katika mambo yote.




Mungu aweza kukufanikisha katika mambo yako. Wengi wanapokutana na changamoto au ugumu katika maisha yao hukimbilia kutafuta suluhisho mahali pasipo sahihi.
Ndiyo maana neno linasema.
"Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama uendavyo katika kweli."
~3John 1:2-3.
Yaani ukisoma utaona Kitu ya kwamba ili ufanikiwe inabidi ufanikiwe kwanza rohoni. Baraka hii ya kufanikiwa katika Kila jambo ipo wazi sana imewalenga wale watakao kula na kushiba na kupata afya katika utu wao wa ndani.
Ndiyo maana Yesu alisema...
"Bali utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake, na hayo yote mtazidishiwa" ~Mathayo 6:33
Kwahiyo kwa lugha nyepesi. ikiwa Unamtegemea Mungu katika kufanikiwa kwako unatakiwa ujibidiishe katika kishibishisha roho yako mambo ya rohoni.
Hivyo Mungu atakufanikisha kwa kukupatia kibali na Ă‘eema katika mambo yote utakayo taka kufanikiwa (Yasiyo chukizo machoni pa Bwana).
Mungu atakupa akili katika Mambo Yote.
neno linasema...
"Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote."
~2 Timotheo 2:7.
Mungu atakupa akili katika mambo yote utakayo taka kuyafanya na utafaulu na kufanikiwa katika Mambo yote.
Katika Jina la Yesu
ufanikiwe katika mambo yako yote
Kama ulivyo fanikiwa rohoni.
Amen.
_________________
Minister: Enoch Joseph
Life word Ministry
+255686909191
©2017

No comments:

Post a Comment

Urithi wa watumishi wa Mungu

URITHI WA WATUMISHI WA MUNGU. ------------------------------------------------------------ Hii wengi hawafahamu lakini leo fahamu japo k...