Thursday, 7 September 2017

Discove the hidden Tressure. Vumbuwa hazina iliyo fichwa.





Shalom shalom.
Kwa mda sasa kulikuwa na Changamoto ya kuleta neno la Mungu. Yesu ametushindia na sasa Tupo Mahali hapa Tena kwa Utukufu wa Bwana. Na injiri itazidi kusonga Mbele. Zakaria 4:7
_______________________________________________
Kabla ya kuenda kwa undani kwenye ujumbe wa leo.
Naomba ufahamu kwa Lugha nyepesi Mambo matatu.
i)Wokovu/Kuokoka
ii) Maisha ya wokovu
iii) Ufalme wa Mungu.
Ukijuwa haya utaelewa neno kwa uzuri sana. Kuokoka au kuokolewa ni kusaidiwa na kutolewa mahali hatarishi na kukuweka mahali salama kwako kuishi. Kuokolewa unaweza okolewa kwa Fedha Mfano Mtu akitekwa Watekaji wanaweza sema leteni fedha ili Tumuachie huyu tuliye mteka, Unaweza okolewa kwa mali, na unaweza okolewa kwa Damu Pia.
Sisi tumeokolewa kwa Damu ya thamani kuliko fedha,dhabu na vitu vinavyo haribika. Na Tumewekwa mahali salama Kuishi na ni upande wa Ushindi.
Neno linasema...
"Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja
naye katika ulimwengu wa roho, katika Yesu;
Kristo" ~ Effeso 2:6
kwahiyo tulio okoka tumeketishwa pamoja na Bwana Yesu katka ulimwengu wa roho.
lakini si tuu ivyo neno linasema...
" akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia"
~Effeso 1:20-21.
Yaani kitendo cha kuokoka unapatiwa heshima kubwa sana. Kuketishwa pamoja na Bwana siyo jambo dogo. Lakini unakuwa juu ya falme,Sultani, na Majina yatajwayo. Unafanya kazi na Bwana Yesu huku Mkiwa mmeketi Pamoja Na Bwana Yesu Kwenye Kiti chenye Mamlaka Juu Ya Falme zote za Dunia hii, na mamlaka zote, na Nguvu na Usultani.
My Friend...
Neno linasema...
" kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi."
~ Ufunuo 5:9-10.
Yesu Damu Yake ili wafanya imetufanya tulio okoka kuwa wafalme na Makuhani tunamiliki juu ya Nchi.
Mtu anapo oko anakuwa ametolewa toka ufalme wa giza yaani Mautini na Kupelekwa ufalme wa Nuru yaani Uzimani nao walio okoka wanampenda Yesu. na Yesu alisema Ukinipenda utalishika Neno langu. kwahiyo kumpenda Yesu ni Pamoja na Kulishika Neno lake.
Maisha ya Wokovu ni mfumo wa maisha ya kifalme ndani ya Yesu. Na katika ufalme wa Mungu Yesu ni Mfalme. Kwahiyo kuokoka ni kuacha mfumo wa Maisha ya utawala wa shetani na kuishi maisha ya Mfumbo wa utawala wa Yesu .
Mfumo wa Maisha ni namna unawaza, namna unavonena, namna unavaa, namna unakula na kila kitu kinacho kuhusu maishani mwako. Katika Ulimwengu wa Nuru Kila lifanyikalo kwa neno au kwa Tendo tunalifanya katika Jina la Yesu.
Mungu anatupenda na kila aliye aliye wake iko hazina ambayo imefichwa kwaajiri yake. Kwahiyo kunavitu adui hana access navyo kwani Bwana amevificha kwaajiri yetu. lakini pia kuna wana wa Mungu waliziona hazina zao kisha wakazitangaza na adui akawanyanganya na kuzifunga kwenye vyumba vyenye makufuri ya shaba Bwana atakwenda Kuvifungua Katika Jina la Yesu.
lakini kuna Mambo ya Msingi unapaswa kufahamu ya kwamba
kama Mwana wa Pendo lake Yesu unapaswa kujuwa Yesu alisema....
" Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa."
Mathayo 7:7-8
Omba Mungu akupe Hazina Iliyo fichwa Gizani na Mahali pa siri Bwana Mungu akupatie Katika Jina la Yesu. Maana kila aombaye Kwa Yesu Hupewa.
Kwa Msaada wa Mungu na kwa Nguvu za Roho Mtakatifu tafuta hazina ya Thamani iliyo fichwa na iliyoo Gizani. maana itayapa thamani Maisha Yako. Maana kila atafutaye kwa Msaada wa Bwana hupata atafutacho.
Ikiwa hazina Yako imeibwa na adui na Kufichwa kwenye vyumba vyenye milango ya shaba Bwana Yesu anakwenda Kuvunja Milango hiyo na hazina hiyo unakwenda kuipata katika Jina La Yesu.
na ufahamu kuwa hii ni ahadi kwa watumishi wa Mungu. na pengine unaweza ukajiuliza ivi mimi pia ni Mtumishi wa Mungu? Yes utumishi wa Mungu ni ni kufanya kile ulicho itiwa na kuaminiwa na Bwana kwa mahali ulipo ukitenda sawasawa na apendavyo Bwana. alipo Mwenye haki wa Bwana watu hufurahi. Tenda haki mahali ulipo. lakini pia Tambuwa Unaweza Ukawa mtumishi wa Madhabahuni na pia unaweza ukawa Msaidizi au mfadhili wa kazi Ya Bwana. Mahali kuna uhitaji ili kazi ya Bwana Isonge Mbele Unaisapoti kazi ya Mungu Kwa hali na Mali. kazi hiyo watu watakapo barikiwa tambuwa na wewe umeshiriki kuifanya kazi ya Bwana.
ndiyo maana neno linasema...
" Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!"
~ Marko 10: 14-15
kwahiyo wanao wapeleka watumishi kuhubiri kwa njia Yeyote ile wanakuwa ni sehemu ya walio Hubiri hivyo nao huitwa Watumishi. Na Mungu anawaheshimu sana.
sasa Yesu alisema...
" Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele."
~ Mathayo 19:29
Yesu amesema Mwenyewe kwa kinywa chake kuwa watumishi wake watapata mara mia hapa Duniani.
ndiyo maana unapaswa ufahamu ya kuwa ipo hazina ya thamani kwaajiri yako iliyopo mahali pa siri au gizani. Bwana anakwenda kukupatia katika Jina la Yesu.
" Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lilo. Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri; naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua."
~ Mathayo 13: 44-46
Yesu alipo toa mfano huu unapaswa kufahamu ulikuwa ni mfano Bora kwake kuufananisha na ufalme wa Mungu. na fahamu ni kwamba ilikuwa imekwisha tokea kwa watu wa namna hiyo au aliona watatokea watu wa namna hiyo baadaye.
ona vitu vya kujifunza.
Uwe na uhakika Ukiomba kwa uaminifu Bwana atakuonesha hazina yenye thamani mara Mia na mara elfu zaidi ya ulivyo navyo. utakapo iona usiende kutangaza kwa watu. ifiche kwanza kisha nenda kauze ulivyo navyo kisha ukainunue.
unajiuriza ukauze nini?
uza ujuzi ulio nao. kafanye vibarua, kafanye kazi, unavitu labada una mifugo, nguo viatu, na biashara ambayo haina faida kubwa kuliko hazina hiyo uliyo iona ...kisha ukainunue. mtaji utakuwa Mshahara, posho na fedha ulizopata baada ya kuuza vinavyo uzika ulivyo navyo.
kwahiyo katika mfano wa Yesu hakuna aliye kwenda kukopa. bali aliuza alivyo kuwa navyo.
namuomba Mungu akakupe Kibarua katika Jina la Yesu ili Upate Mtaji na Fedha ya Kulinunua shamba Lenye kito cha thamani katika Jina la Yesu.
Namuomba Mungu akupe wateja wa Kununua ulivyo navyo ili ukapate weza kuinunua lulu iliyo na thamani mara kumi elfu kuliko mali ulizo nazo kwa Jina la Yesu.
na pia kwaajiri yako wewe Mtumishi wake Mungu.
Bwana Yesu anasema.
"Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma;nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli. Kwa ajili ya Yakobo, mtumishi wangu, na Israeli, mteule wangu, nimekuita
kwa jina lako; nimekupa jina la sifa; ijapokuwa
hukunijua".
~ Isaya 45 :2-4
Mungu anakwenda Kuyavunja Makufuri na Mirango ya Shaba. ukaipate hazina yako.
Mungu anakwenda kukatakata mapingo ya Chuma.
Mungu anakwenda kukupa Hazina za Gizani na mali zilizofichwa za mahali pa siri.
Nawe utajuwa ya Kwamba aliyetenda Ni Bwana akuitaye kwa Jina lako na ni Mungu wa Israeli.
katika Jina la Yesu.
kwa Msaada Wa Bwana Ufanikiwe.
Katika Jina la Yesu na Iwe kwako kama Bwana alivyo sema.
Amen.
__________________________________
Minister Enoch Joseph
Life word Ministry
@ 2017

No comments:

Post a Comment

Urithi wa watumishi wa Mungu

URITHI WA WATUMISHI WA MUNGU. ------------------------------------------------------------ Hii wengi hawafahamu lakini leo fahamu japo k...